Aveva, Kaburu waendelea kung'ang'aniwa...soma habari kamili na Matukio360..#share
Na
Abdulrahim Sadiki
JALADA
la uchunguzi la kesi ya utakatishaji fedha wa USD 300,000, inayomkabili rais wa klabu
ya Simba, Evans Aveva na makamu wake, Godfrey Nyange ‘Kaburu’ bado lipo kwa mkurugenzi wa mashtaka ,(DPP).
Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva wa mbele na makamu wake, Godfrey Nyange ‘Kaburu’
Leo
wakili mkuu wa serikali, Vitalis Peter ameeleza hayo kwa Hakimu Mkazi
Mwandamizi, Victoria Nongwa na kuwa kesi hiyo ilipangwa kutajwa lakini jalada la uchunguzi bado lipo kwa DPP. Ameomba
kesi hiyo ipangiwe tarehe nyingine.
Hata
hivyo wakili wa washtakiwa, Evodius Mtawala ameiomba mahakama iwasisitize
upande wa mashtaka kuitilia mkazo kesi hiyo. Hakimu Nongwa ameahirisha
kesi hiyo hadi Novemba 10,2017.
Evans Elieza Aveva na makamu wake, Geofrey wanakabiliwa na
mashtaka matano ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha fedha
USD 300,000.
Katika shtaka la
kwanza, washtakiwa hao wanadaiwa kuwa
walikula njama ya kughushi fomu ya maombi ya kuhamisha fedha ya Machi
15,2016 wakionesha Klabu ya Simba inalipa mkopo wa USD 300,000 kwa Evans Aveva wakati si kweli.
Katika shtaka la pili
alidai kuwa Machi 15,2016 katika benki ya CRDB tawi la Azikiwe Ilala Aveva
akijua alitoa nyaraka za uongo ambayo ni fomu ya maombi ya kuhamisha fedha ya
Machi 15,2016 wakati akijua ni kosa.
Katika la tatu la
kutakatisha fedha, Aveva na Nyange wanadaiwa kuwa kati ya Machi 15 na Juni
29,2016 Dar es Salaam kwa pamoja
walikula njama ya kutakatisha fedha kwa kupata USD 300,000 wakati wakijua ni
zao la uhalifu.
Kwa upande wa shtaka
la nne la kutakatisha fedha, Aveva anadaiwa kuwa kati ya Machi 15,2016 katika
benki ya Baclays Mikocheni alijipatia USD 300,000 wakati akijua zimetokana na
kughushi.
Katika shtaka la tano
la kutakatisha fedha, mshtakiwa Nyange anadaiwa kuwa Machi 15,2016 katika benki ya Baclays tawi la
Mikocheni alimsaidia Aveva kujipatia USD
300,000 wakati akijua fedha hizo zimetokana na kughushi. Washtakiwa wapo
rumande kwa sababu shtaka la kutakatisha fedha linalowakabili halina dhamana.
No comments:
Post a Comment