'UPDATES' Zitto, kamati kuu ACT waripoti Polisi....soma habari kamili na Matukio360..#share
Na mwandishi wetu
VIONGOZI wa chama cha
ACT Wazalendo, leo wameripotia katika vituo viwili tofauti vya polisi jijini Dar es
Salaam.
Kaimu katibu mkuu ACT Wazalendo, Dorroth Semu akifika katika kituo cha makosa ya uchunguzi wa kifedha eneo la Kamata
Saa nne asubuhi kaimu katibu mkuu wa ACT Wazalendo, Dorroth Semu na mwenyekiti, Yeremia Maganja wamewasili katika kituo cha makosa ya uchunguzi wa kifedha eneo la Kamata
Saa nne na nusu Zitto Kabwe
akiwa na mawakili wawili amewasili kituo cha Chang’ombe kujua hatma kama
atafikishwa mahakamani au uchunguzi dhidi yake bado haujakamilika.
Zitto anatuhumiwa
kufanya makosa ya uchochezi huku kamati kuu ya ACT Wazalendo ikituhumiwa kwa
kutoa takwimu za uchumi kinyume cha sheria na utaratibu.
Afisa Habari wa ACT
Wazalendo, Abdallah Khamis ameiambia Matukio360 kuwa Zitto ameambata na mke
wake na baadhi ya viongozi wa chama
hicho.
Huku kaimu mwenyekiti
na katibu nao wameongozana na mwanasheria Michael Mboya.
Miongoni
mwa makosa aliyoojiwa Zitto ni kwamba Jumapili ya Oktoba 29, 2017 alipokuwa kwenye mkutano wa
kuzindua kampeni za udiwani katika Kata ya Kijichi, Wilayani Temeke alitoa
maneno yanayoweza kupelekea uvunjifu wa amani. Maneno hayo ni yafuatayo:
1.
Kwamba wananchi wasiichague CCM kwa sababu Serikali yake imeshindwa kufanya
uchunguzi na kuwakamata watu waliompiga risasi Mbunge Tundu Lissu mpaka siku
hiyo.
2.
Kwamba wananchi wasiichague CCM kwa sababu Serikali yake imeshindwa kueleza
chanzo cha miili ya watu wanaookotwa kwenye fukwe za bahari kama Coco Beach.
Hivyo kuichagua CCM ni sawa na kuwaunga mkono waliofanya vitendo vya
kumshambulia Tundu Lissu na wanaoua watu wanaookotwa kwenye fukwe.
Kaimu katibu mkuu ACT Wazalendo, Dorroth Semu akipanda kwenda katika chumba cha mahojiano katika kituo cha makosa ya uchunguzi wa kifedha eneo la Kamata leo jijini Dar es salaam
No comments:
Post a Comment