'UPDATES' Zitto Kabwe atakiwa kuripoti Polisi Ijumaa ijayo...soma habari kamili na Matukio360..#share

Na mwandishi wetu
JESHI la Polisi limemtaka kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe kuripoti tena katika kituo cha Chang’ombe Ijumaa ya Novemba 17, 2017

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe
Alifika kituoni hapo mapema leo kufuatia wiki iliyopita kuhojiwa  na Polisi  akituhumiwa kufanya makosa ya uchochezi.

Akizungumza na Matukio360 mara baada ya kutoka kituoni hapo, Zitto amesema kinachosubiriwa ni jalada la  maelezo  kutoka kwa mkurugenzi wa makosa ya jinai (DCI) kwenda kituoani hapo na kwamba uenda hadi kufikia Ijumaa litakuwapo

Awali Afisa Habari wa ACT Wazalendo, Abdallah Khamis ameiambia Matukio360 kuwa leo Zitto akiambata na mkewe na baadhi ya viongozi wa ACT alifika ili kujua hatma kama atafikishwa mahakamani au uchunguzi dhidi yake bado haujakamilika.

Miongoni mwa makosa aliyohojiwa ni kwamba Jumapili ya  Oktoba 29, 2017 alipokuwa kwenye mkutano wa kuzindua kampeni za udiwani katika Kata ya Kijichi, Wilayani Temeke alitoa maneno yanayoweza kupelekea uvunjifu wa amani. Maneno hayo ni yafuatayo:

1. Kwamba wananchi wasiichague CCM kwa sababu Serikali yake imeshindwa kufanya uchunguzi na kuwakamata watu waliompiga risasi Mbunge Tundu Lissu mpaka siku hiyo.


2. Kwamba wananchi wasiichague CCM kwa sababu Serikali yake imeshindwa kueleza chanzo cha miili ya watu wanaookotwa kwenye fukwe za bahari kama Coco Beach. Hivyo kuichagua CCM ni sawa na kuwaunga mkono waliofanya vitendo vya kumshambulia Tundu Lissu na wanaoua watu wanaookotwa kwenye fukwe.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search