CCM ilimvua uanachama Nyalandu, Spika Ndugai athibitisha...soma habari kamili na Matukio360..#share
Na
mwandishi wetu
OFISI
ya Spika wa Bunge imesema Lazaro Nyalandu si mbunge tena na hatua stahiki za
kuiarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi(Nec) zinaendelea kuchukuliwa.
Imesema
hatua hiyo inafuatia katibu mkuu wa CCM kuiandikia ofisi ya Bunge barua
ikimualifu kwa muda CCM ilishaanza kumchukulia hatua kiudhibiti na kinidhamu
dhidi ya vitendo na kauli za Nyalandu zisizoridhisha kinyume na misingi,
falsafa na itikadi ya chama hicho.
Hivyo
kuanzia tarehe ya barua hiyo ya Oktoba 30, 2017 Nyalandu amepoteza sifa za
uanachama wa CCM na kupoteza nafasi zote za uongozi wa ndani wa chama hicho na
ubunge kwa mujibu wa ibara ya 13 ya CCM.
Hatua
hiyo inafuatia baada ya hivi karibuni Nyalandu kutangaza kujiuzulu ubunge na
kung’atuka CCM
No comments:
Post a Comment