NEC: Uchaguzi udiwani kutumia bilioni 2.5.....soma habari kamili na Matukio360...#share
Na
mwandishi wetu
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema katika uchaguzi mdogo
wa madiwani utakaofanyika Novemba 26, 2017 katika kata 43 utagharimu kiasi cha
bilioni 2.5.
Mkurugenzi wa Uchaguzi Ramadhani Kailima kulia akiwa na mkurugenzi aliyemaliza muda wake, Jaji Julius Mallaba (kushoto), ambaye aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania
Pia
imepokea rufaa 14 kutoka kwa wagombea ambao hawakuridhika na maamuzi
yaliyotolewa na wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo na kwamba rufaa zitasikilizwa Ijumaa ya Oktoba 3 na Jumatatu ya Oktoba 6,2017 itatoa uamuzi.
Mkurugenzi
wa Uchaguzi wa NEC, Ramadhani Kailima, amesema hayo leo jijini Dar es salaam lipokuwa akizungumzia
maandalizi ya Uchaguzi huo wa Madiwani utakaofanyika Novemba 26, 2017.
Amesema
msingi wa bajeti ya uchaguzi unategemea idadi ya vituo vya kupigia kura na
idadi ya wapiga kura waliokuwepo katika kata husika.
Amesema
idadi ya watu ndio inatoa bajeti ya karatasi za kupigia kura pamoja na vituo
ambavyo vinakuwa na watumishi wasiopungua wanne.
Kailima
amesema katika kituo cha kupigia kura kina watumishi msimamizi wa kituo,
msaididzi, karani mwongozaji na mlinzi wa kituo “lakini pia kuna watu wa ziada
wako ngazi ya kata na jimbo ambao wanaweza kutumika iwapo msimamizi wa kituo na
msaidizi wake wameapata dharura.
Amesema
kata yenye vituo 40 ina bajeti kubwa kuliko kata yenye vituo vichache. Amesema
bajeti hiyo pia inategemea askari wanaosimamia uchaguzi na umbali ambako uchaguzi
huo unafanyika.
Amefafanua
gharama zingine za uchaguzi ziko kwenye
usafirishaji wa vifaa kwenda kwenye kata ambako uchaguzi unafanyika pamoja na
machapisho mbalimbali yatakayotumika kwa ajili ya kutoa elimu ya mpiga kura.
Wakati
huo huo NEC imevitaka vyama vya siasa na wagombea wanaoshiriki uchaguzi mdogo
wa madiwani kutekeleza na kuheshimu maadili ya Uchaguzi na kuonya kuwa chama au
mgombea atakayekiuka maadili hayo atachukuliwa hatua kama ilivyoanishwa chini
ya Kifungu cha 124A cha Sheria ya Uchaguzi Na.1 ya mwaka 1985.
Amevitaka
vyama vya siasa kuhakikisha kuwa vinawaelemisha wafuasi wao juu ya kutekeleza
maadili hayo katika kipindi chote cha kampeni.
Aidha,
amesema iwapo wafuasi wa vyama vya siasa
watavunja maadili hayo, chama husika pamoja na mgombea wake kitachukuliwa hatua
za kinidhamu.
Mkurugenzi
Kailima amevitaja vitendo vinavyokiuka maadili ya uchaguzi kuwa ni pamoja na
wagombea au wafuasi wa vyama hivyo kuchana mabango ya wagombea wengine, kutoa
lugha chafu wakati wa mikutano ya kampeni pamoja na kupitisha muda wa kufanya
mikutano ya kampeni.
Amezitaka
kamati za maadili za kata na jimbo kuchukua hatua kali kwa chama au mgombea
ambaye atavunja maadili hayo.
Amesema
kamati hizo zinatakiwa kuchukua hatua ndani ya saa 48 mara chama au mgombea
anapovunja maadili.
Amesema
kuwa miongoni mwa adhabu zinazowakabili wagombea au chama ambacho kitakiuka
maadili ya uchaguzi ni kuomba radhi wananchi hadharani, kutotumia vyombo vya
habari kwa muda fulani, onyo la maandishi kusimamishwa kufanya kampeni, mgombea
kutangaza mbele ya vyombo vya habari kuwa yeye ni bingwa wa kuvunja maadili ya
uchaguzi au kutozwa faini Sh 100,000.
Kailima
pia amesema chama cha siasa ambacho kinataka kufanya mabadiliko ya ratiba ya
mikutano ya kampeni, lazima kimfahamishe msimamizi wa uchaguzi wa kata na ombi
hilo lazima lijadiliwe na vyama vyote vinavyoshiriki kwenye uchaguzi.
Kuhusu
vitambulisho mbadala vitakavyotumika wakati kupigia kura kwa wale ambao
wamepoteza kadi ya mpiga kura ambavyo ni vitambulisho vya taifa, leseni ya
udereva na hati ya kusafirisha; Kailima amesema vitambulisho hivyo vitatumika
tu kwa watu ambao wameandikishwa katika kituo husika mwaka 2015, lakini pia
bado wana sifa za kupiga kura.
Amesema
vitambulisho hivyo vitatu hata kama vimeisha muda wake, mhusika anaruhusiwa
kupiga kura.
“Pale
tunachoangalia ni uthibitisho wa mtu sio kwamba anasafiri au anaendesha gari,
pia tunaamini kuwa vimetolewa na mamlaka husika.
Kailima
ametoa mwito kwa vyama vya siasa kutambua kwamba tume ya taifa ya uchaguzi
imeruhusu mikutano ya kampeni na sio mikutano ya vyama vya siasa.
Amesema
mtu anayeruhusiwa kwenye mikutano ya kampeni ni mgombea mwenyewe, chama chake
au mtu yeyote ambaye anaona anaweza kumfanyia kampeni ndani ya katiba
iliyopitishwa.
No comments:
Post a Comment