Kesi 'Mpemba wa Magufuli' kuhamia mahakama ya mafisadi...soma habari kamili na Matukio360..#share
Na Abdulrahim Sadiki
KESI
ya kujihusisha na biashara haramu ya meno ya tembo inayomkabili mfanyabiashara
Yusuf Ali ‘Mpemba wa Magufuli’ na wenzake watano inatarajiwa kupelekwa katika Mahakama
Kuu Kitengo cha Rushwa na Uhujumu Uchumi 'Mahakama ya Mafisadi'
Meno ya tembo
Wakili
wa Serikali, Elizabeth Mkunde ameyaeleza
hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,
Thomas Simba. Hatua hiyo imefikiwa
baada ya upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi wa kesi hiyo. Hata hivyo kesi
imeahirishwa hadi Novemba 15,2017.
Mbali
ya Mpemba, washtakiwa wengine ni Charles
Mrutu, mkazi wa Mlimba, Morogoro, Benedict Kungwa, mkazi wa Mbagala Chamazi,
Jumanne Chima, mkazi wa Mbezi, Ahmed Nyagongo, dereva na Pius Kulagwa.
Washtakiwa
hao wanakabiliwa na mashtaka manne ya
kujihusisha na biashara ya meno ya tembo yenye thamani ya milioni 785.6.
Inadaiwa
katika tarehe tofauti kati ya Januari, 2014 na Oktoba, mwaka huu wakiwa Dar es
Salaam, Tanga, Iringa na Mtwara, walijihusisha na mtandao wa ujangili kwa
kukusanya na kuuza nyara za serikali ambazo ni vipande vya meno ya tembo 50
vyenye thamani ya Dola za Marekani 180,000 sawa na milioni 392.8 bila kuwa na
kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori.
Oktoba
26, 2016, washtakiwa hao wakiwa Mbagala Zakhem, walikutwa na vipande vya meno
ya tembo10 vyenye uzito wa kilo 13.85
vya thamani ya dola za Marekani 30,000 sawa na milioni 65.4
Wanadaiwa
kuwa Oktoba 27,2016 wakiwa Tabata
Kisukuru washtakiwa hao walikutwa na vipande vinne vya meno hayo ya tembo yenye
uzito wa kilo 11.1 na thamani ya dola za Marekani 15,000 sawa na milioni 32.7
Pia
Oktoba 29,2016 walikutwa na vipande 36 vya thamani ya milioni 294.6 bila kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa
Wanyamapori.
No comments:
Post a Comment