Diamond 'ambwaga' Mobeto...soma habari kamili na Matukio360..#share
Na Mwandishi wetu
MAHAKAMA ya Hakimu
Mkazi Kisutu upande wa Watoto imeitupilia mbali kesi iliyofunguliwa na mwanamitindo,
Hamisa Mobeto dhidi ya mwanamuzi, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnum’. Hata hivyo, Mobeto anaratajia kukataa rufaa dhidi ya hukumu hiyo
Msanii, Naseeb Abdul 'Diamond Platnum'
Hata hivyo, Mobeto
anaratajia kukataa rufaa dhidi ya hukumu hiyo
Uamuzi huo umetolewa
leo na Hakimu Devotha Kisoka wa mahakama hiyo.
Hakimu Devotha ametoa
uamuzi huo baada ya kusikiliza hoja za pande hizo mbili husika kutokana na msanii Diamond kuwasilisha
pingamizi dhidi ya kesi hiyo iliyofunguliwa na Mobeto.
Kwa mujibu wa
pingamizi lililowasilishwa na
Diamond mahakamani hapo anadai
kuwa kesi hiyo imefunguliwa kwa kutumia
kifungu ambacho si sahihi. Hoja ambayo
ilipingwa na Mobeto.
Mobeto alifungua kesi
hiyo mahakamani hapo, pamoja na mambo mengine aliomba matunzo ya mtoto waliozaa
na msanii Diamond.
Mobeto aliiomba mahakama imwamuru Diamond kutoa
matunzo ya mtoto ya kila mwezi na alifungua kesi hiyo kupitia mawakili wake
Abdullah Lyana na Walter Godluck kutoka kampuni ya uwakili ya Century
Attorneys.
Kupitia hati hiyo ya
madai, Mobeto anaomba Diamond amuombe
msamaha kwa kumsababishia madhara yaliyoishtua familia yake.
Diamond aliwasilisha hati ya majibu hayo
kinzani akipinga maombi hayo ya Mobeto
akidai gharama anazodai kulipwa kwa
mwezi ya milioni 5 kwa ajili ya matunzo
ya mtoto ni kubwa hawezi kuzimudu.
No comments:
Post a Comment