StarTimes yaja na 'Mfalme wa Familia'...Soma habari kamili na Matukio360..#share
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI
ya Star Media (T) Ltd kupitia chapa yake ya StarTimes katika msimu huu wa Sikukuu
imekuja na Ofa ya aina yake ijulikanayo kama ‘Mfalme wa Familia’ kwa ajili ya
wateja watakaopenda kujiunga na huduma za kampuni hiyo.
Meneja Uhusiano na Masoko wa kampuni hiyo Juma Suluhu.
Hayo
yamebainishwa jijini Dar es Salaam na Meneja
Uhusiano na Masoko wa kampuni hiyo Juma Suluhu akizungumza na waandishi wa
habari, amesema StarTimes inatambua
umuhimu na uzito wa kipindi hiki cha sikukuu kwa watanzania hivyo wamejipanga
vyema kutoa burudani ya kiwango cha hali ya juu.
“Tumewaletea
watanzania Ofa tuliyoipatia jina la ‘Mfalme wa Familia’, tumeiita hivyo kwa
sababu sisi ni wafalme wa Burudani za Familia, ukianzia filamu, michezo kama
mpira wa miguu, kikapu, katuni, Muziki, Ndondi na vingine vingi. Tuna vipindi
ambavyo watoa huduma wengi hawana, hivyo ni fursa ya kipekee kwa watanzania
kufurahia,” amesema Juma.
Aidha
ameongeza kuwa ofa hiyo inaenda sambamba na kushuka bei ya king’amuzi cha
Antenna ambacho awali kilikuwa kikiuzwa kwa Tsh 47,000 ambacho kwa wakati hua
kitapatikana kwa bei ya punguzo ya sh. 34,000 .
“Ofa
yetu ina mambo makubwa matatu, Jambo la kwanza ni hilo punguzo la bei ya
king’amuzi cha Antenna, pili ni king’amuzi cha Combo ambacho kinatumia dish na
Antenna ambacho awali kilikuwa kikiuzwa kwa Tsh 86,000 sasa kitapatikana kwa
Tsh 78,000 huku mteja atakayenunua atapata kifurushi cha Mwezi mzima pamoja na
Dish Bure”, amesema Juma.
“Tatu
ni luninga zetu za kidigitali, hapa unapata vitu vitatu, cha kwanza luninga
zetu zina king’amuzi ndani, cha pili ukinunua luninga yetu unapatiwa dish bure
na cha mwisho utaunganishwa kifurushi cha Uhuru kwa mwezi mmoja Bure”, ameongeza.
Licha
ya ofa hizo wateja wa StarTimes wataweza kupata Chaneli zote za Kifurushi cha
Kili katika kifurushi cha Uhuru kuanzia Disemba 1, 2017 ikiwa ni sehemu ya Promosheni
ya Mfalme wa Familia ambayo imeletwa na StarTimes Tanzania.
No comments:
Post a Comment