Meya Mwita ahudhuria mkutano tabia nchi...Soma habari kamili na Matukio360..#share
NA CHRISTINA MWAGALA
MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amesema kuwa
mkutano wa COP 23 ambao Mameya na watendaji wakuu wa majiji na miji
mbalimbali duniani utatoa suluhisho la pamoja la kukabiliana na
changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi katika miji yao.
Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita katikati mwenye koti jeusi , Mkurugenzi wa jiji Sipora Liana wa kwanza kulia wakijadiliana jambo na ujumbe wa jiji la Hamburg katika mkutano wa mabadiliko ya Tabia ya Nchini unaoendelea Nchini Ujerumani.
Akiwa Nchini Ujerumani , Meya Mwita emesema kuwa mkutano huo
utakuwa mahususi kwa jiji la Dar es asalaam kupata suluhisho na
kuhakikisha kuwa wanakabiliana ipasavyo na mabadiliko ya tabia ya
nchi ikiwemo janga la mafuriko ambalo limekuwa ni tatizo sugu jijini hapa.
Mkutano huo unaofanyika sambamba na Mkutano wa 23 wa Umoja
wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabia ya Nchi, COP 23 inahusu miji na Taasisi
zenye uhusiano na ubia na miji ya Ujerumani katika utekekezaji wa miradi ya
kukabiliana na mabadiliko hayo inayofadhiliwa na Nchi hiyo.
Mkutano huo wa kimataifa wa Mabadiliko ya Tabia ya Nchi
umeandaliwa na Taasisi ya Engagement Global ya Ujerumani kwa miji washirika
kutoka nchi mbalimbali duniani ambapo umeanza jana alasiri mjini Bonn
nchini Ujerumani.
Kutoka Tanzania miji mingine inayoshiriki katika mkutano huo ni
Jiji la Mwanza, Manispaa ya Zanzibar na Halmashauri ya Wilaya ya Masasi.
Hata hivyo mkutano huo utaendelea hadi Novemba 11, mwaka huu
ambapo jiji la Dar es Salaam linashiriki katika likiwa na ujumbe
wake unao ongozwa na Mstahiki Meya Jiji hilo Mwita pamoja na
Mkurugenzi Sipora Liana.
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita katikati mwenye koti jeusi ,akiwa na Mkurugenzi wa jiji Sipora Liana wakipata chai baada ya kumaliza awamu ya kwanza ya mkuanomhuo.
No comments:
Post a Comment