Diamond 'matatani' kuilipa Msondo Ngoma milioni 300...soma habari na Matukio360..#share
Na Mwandishi Wetu
BENDI ya Muziki wa Dansi ya Msondo Ngoma imeipa siku saba
Kampuni ya Muziki wa Kizazi Kipya ya Wasafi Classic Baby (WCB) iliyoko chini ya
msaani maarufu nchini,Naseeb Abdul ‘Diamond’ kuilipa milioni 300.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Wasafi Classic Baby (WCB) Naseeb Abdul 'Diamond'.
Kwa mujibu wa barua iliyoandikwa na Mkurugenzi Mwenza wa
Kampuni ya Uwakili ya Maxim Advocates, Mwesigwa Muhingo wanaoisimamia bendi
hiyo ya Msondo Ngoma kwenda kwa Mkurugenzi wa WCB, imeeleza kuwa ni kutokana na
wao kutumia melodi ya wimbo ‘ajali’ unaomilikiwa na Msondo Ngoma katika wimbo
wa ‘Zilipendwa’ bila ruhusa.
Aidha barua hiyo imebainisha kuwa ikiwa WCB itashindwa kulipa
fedha hizo ndani ya muda huo, hatua nyingine za kisheria zitafuata.
Wimbo wa zilipendwa uliimbwa na wasanii waliopo chini ya lebo
hiyo ya WCB, ambao ni Diamond Platnumz, Rich Mavoko, Rayvanny,
Queen Darlin, Maromboso na Lavalava.
Tayari baraza za sanaa (Basata) na lile la haki miliki(Cosota) wamethibitisha kupokea barua ya madai hayo kutoka kamouni ya uwakili ya Maxim
Tayari baraza za sanaa (Basata) na lile la haki miliki(Cosota) wamethibitisha kupokea barua ya madai hayo kutoka kamouni ya uwakili ya Maxim
No comments:
Post a Comment