Uchunguzi haki za binadamu katika biashara wazinduliwa...soma habari kamili na Matukio360..#share
Salha
Mohamed
TUME
ya Haki za binadamu na Utawala Bora, imevitaka vyombo vinavyohusika na sheria
kutekeleza na kusimamia haki za binadamu katika biashara .
Mwenyekiti wa Tume ya haki za binadamu na Utawala
Bora, Bahame Nyanguda(katikati)
akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango wa Uchunguzi wa taarifa wa haki
za binadamu katika biashara nchini leo,
kushoto ni Kamishna wa tume hiyo,
Muhammed Hamis Hamad na Ofisa Uchunguzi Mwandamizi, Jovina Muchunguzi.
Hayo
yamesemwa jijini Dar es Salaam na
Mwenyekiti wa tume hiyo, Bahame Nyanguda alipokuwa akizindua mpango wa uchunguzi
wa taarifa wa haki za binadamu katika biashara.
Amesema
kuzinduliwa kwa taarifa hiyo utawezesha kuangalia biashara zinazozingatia haki
za binadamu nchini.
"Mwaka
2013 serikali iliandaa mpango kazi wa haki za binadamu nchini ambao unaratajia
kukamilika Disemba mwaka huu ambao umeainisha masuala ya namna ya kusimamia,
kulinda, kuheshimu na kutetea haki za
binadamu katika kipengele cha biashara, "amesema.
Amesema
katika biashara kipengele cha haki za binadamu hakikutekelezwa katika kipindi
cha miaka 4 iliyopita na kuamua kuandaa mpango kazi utakaosimamia haki za
binadamu katika biashara.
Amesema
umoja wa mataifa umekubaliana na malengo endelevu kuzingatia haki katika masuala
ya biashara, maendeleo ya ukuaji wa uchumi, haki za kijamii ambazo zinaguswa na
biashara.
Ameongeza
umoja wa mataifa ulizitaka kampuni binafsi
zinapowekeza ziweze kuisaidia
jamii kwani ilionekana kujitolea katika huduma za kijamii haitoshi.
Amesema
watu wamekuwa na dhana potofu kwamba kampuni haihusiki katika uvunjaji wa haki
za binadamu nakubainisha kwamba kampuni inaweza kuhusika na zinaweza
kuchukuliwa hatua za kisheria ilimradi taasisi zinazohusika na utekelezaji wa
Sheria ufanye hivyo.
"Wasikubali
udhaifu huo ni lazima haki za binadamu zifuatwe.. .. Sheria zipo na mara nyingine utekelezaji wake ni hafifu, "amesema.
Kwa upande wake ofisa
uchunguzi Mwandamizi wa tume hiyo,
Jovina Muchunguzi amesema katika taarifa hiyo waliibua changamoto zinazoonesha
uhalisia ambayo yamepangiwa utekelezaji wake.
"Tunaamini
tutafika kwenye kutatua changamoto ambazo zimelengwa hasa kwenye Viwanda,
uchimbaji madini, kilimo, utalii na biashara, "amesema.
Akizungumzia athari
ambazo wameziona katika uchunguzi huo, Kamishna wa tume hiyo, Muhammed Hamis Hamad amesema changamoto ipo kwenye sekta ya utalii.
" Tumeangalia
katika sekta ya utalii Zanzibar, lakini tumeangalia athari kwa binadamu na
changamoto zipo si kwa watembeza watalii tu lakini hata kimazingira,
"amesema.
Amesema kumekuwa na
uharibifu wa mazingira katika sehemu za makazi ya watu kwa kujengwa hoteli huku
miundombinu ikiwa haiboreshwi.
" Lazima
tuangalie lakini pia kuna uvunjifu wa haki za binadamu kwa watu kupata
matatizo, ghasia, takataka masuala ya usalama ingawa utalii unachangia kwenye
pato la taifa, "amesema.
Ameongeza kuwa
uzinduzi wa uchunguzi huo ni mpya nchini
huku akibainisha kutokuwepo kwa sheria ya makampuni kuisaidia jamii.
" Nchi zingine
ni lazima kampuni iliyowekeza kuwa na wajibu
wa kuisaidia jamii... Lakini sasa hivi makampuni hufanya kwa hiari
hayalazimishwi kisheria na ndiyo wajibu wao kuisaidia jamii, "amesema.
No comments:
Post a Comment