Dk Ndugulile: TFDA ongezeni 'spidi' katika utendaji ...soma habari kamili na Matukio360..#share
Na Abrahama Ntambara
NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Faustine Ndugulile ameitaka mamlaka ya chakula na dawa (TFDA) kuendeleza mapambano ya kudhibiti uingizwaji wa dawa duni, vifaa tiba na vitenganishi visivyo na ubora nchini.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Fustine Ndugulile kushoto akiwa ameshikana mkono na Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo baada ya Uzinduzi huo jijini Dar es Salaam.
Pia ameitaka TFDA iendelea kuuboresha mfumo wa ubora wa huduma kwa kutenga rasilimali za kutosha, ili kuhakikisha wanendelea kutoa huduma bora za udhibiti kwa kukidhi mahitaji na matarajio ya wateja, bila kuathiri ubora, usalama na ufanisi wa bidhaa wanazodhibiti.
Ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa cheti cha Mfumo wa Uhakiki Ubora wa Huduma kinachoendana na Kiwango cha Kimataifa cha ISO 9001:2015 ambacho TFDA walitunukiwa na Shirika la ISO Agosti 2017 na ISO baada ya ukaguzi wa kina.
Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Hiiti Sillo amesema utekelezaji wa mfumo huo ni chachu
ya maendeleo yaliyofikiwa na mamlaka hiyo.
Amesema Tanzania ni nchi ya kwanza kwa nchi za Afrika Mashariki
kutumia mfumo huo katika kutoa huduma za wazi kwa wadau na wateja wake huku
ikiwa ya pili kwa Afrika ikitanguliwa na Ghana.
“Mfumo huu sasa unatekelezwa katika Kurugenzi na Ofisi zote
za Kanda za TFDA,” amesema Sillo.
Sillo amebainisha kuwa mfumo huo unajumuisha shughuli za
kutengeneza, kufanya marejeo na kusimamia matumizi ya nyaraka, kufanya kaguzi
za ndani kwa kutumia timu ya Wakaguzi wa Ndani wa Mifumo waliofuzu mafunzo ya
ukaguzi.
Nyingine ni kusimamia ukaguzi wa Nje wa Mfumo kwa ajili ya
kupewa cheti cha Usajilicha ISO, kuratibu marejeo ya mfumo yanayofanywa na Menejimenti pamoja na kutekeleza na
kusimamia mfumo wa kusimamia vihatarishi (Risk Management Framework).
No comments:
Post a Comment