Muhimbili, Aga Khan kupandikiza matiti bure...soma habari kamili na Matukio360..#share
Na
Salha Mohamed
HOSPITALI
ya Taifa Muhimbili(MNH), Aga khan na taasisi isiyo ya kiserikali ya Women for
Women wanatarajia kufanya upasuaji na
kuotesha matiti yaliyokatwa kutokana na saratani pamoja na upasuaji kwa watoto walioungua,
bure.
Daktari bingwa wa upasuaji hospitali ya Aga Khan, Dk Aidan Njau akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuanza kwa upasuaji na kupandikiza matiti kwa wanawake waliokatwa kutokana na satarani, kulia ni Daktari bingwa wa upasuaji Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk. Edwin Mrema.
Upasuaji
huo unaoanza leo utahusisha wagonjwa 40 wa kuanzia
Hayo
yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na
Daktari wa Bingwa wa Upasuaji Hospitali ya Aga khan, Dk Aidan Njau alipozungumza
na waandishi wa habari kabla ya kuanza kwa upasuaji huo.
“Mwanamke
anapoambiwa anasaratani ya titi anapata maumivu makali na huathirika kisaikolojia
hasa wanapoambiwa linatakiwa likatwe na wengine huacha na kuwaumiza na
saratani husamba mwilini kisha kufa,”amesema.
Amesema
mwanamke aliyekatwa matiti anakuwa na maumivu zaidi pindi anaporudi kwenye
jamii hujiona yupo tofauti na wenzake kimaumbile.
“Mchakato
huo utakuwa endelevu na wanawake ambao matiti yao yamekatwa wafike hospitali
ili kupata matibabu kwa kuhamisha sehemu ya mwili na kuitengeneza iwe ziwa na
ataendelea kama kawaida hata akivaa nguo itakaa sawa,”amesesma.
Daktari bingwa wa upasuaji MNH, Dk Edwin Mrema
amesema upasuaji huo ni mwendelezo wa hatua za mradi wa taasisi ya Women for
Women na kwamba wanafanya upasuaji kwa wanawake na watoto waliopata ajali ya
moto.
“Wagonjwa
tuliowafanyia upasuaji wamepata mabadiliko wameweza kurudi kwenye jamii awali walikuwa hawawezi kujichanganya kwenye
jamii kutokana na kuungua moto,”amesema
Amesema
ili kuendeleza upasuaji huo wametoa nafasi kwa wanafunzi wa chuo cha Aga Khan
na Muhimbili (Muhas) ili kuwaongezea uwezo wa kufanya upasuaji kwa kushiriki
katika upasuaji huo.
No comments:
Post a Comment