Nape Nnauye avunja ukimya atoa la moyoni...soma habari kamili na matukio360..#share


Na Abraham Ntambara
MBUNGE wa Mtama(CCM) , amesema atokihama   Chama cha Mapinduzi(CCM) na badala yake ataendelea kukisoa akiwa ndani na si nje ya chama hicho.


Nape Nnauye, kushoto akiwa na Lazaro Nyalandu katikati na katibu mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana
 Nape anatoa kauli hiyo  ikiwa ni siku chache baada ya aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki, Lazaro Nyalandu kujiuzulu Ubunge na kung'atuka CCM akisema pamoja na mambo mengine CCM imeshindwa kuidhibiti serikali.
Leo katika ukurasa wake wa twitter Nape ameandika "Chama cha siasa ni ITIKADI, itikadi ni IMANI. Siamini SANA
katika kubadili Imani kienyeji. Nitasghulikia MAPUNGUFU nikiwa ndani sio NJE"8 hours ago

Andiko hilo linaashiria kuvunja ukimya na kudhihirisha kwamba Nnape ambaye aliwahi kuwa waziri wa habari na michezo hatong'oka CCM

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search