Kesi ya Tundu Lissu yaunguruma... soma habari kamili na Matukio360..#share
Na
mwandishi wetu
KESI
ya uchochezi inayomkabili mbunge, Tundu Lissu na wahariri wa gazeti wa la Mawio
imeahirishwa hadi Novemba 30, 2017 kwa sababu Lissu anaumwa. Washtakiwa wengine wote walikuwapo.
Tundu Lissu
Kesi
hiyo ipo katika hatua ya usikilizwaji wa ushahidi wa mashahidi wa upande wa
mashtaka kwa Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.
Leo
wakili wa serikali, Elizabeth Mkunde
amedai kesi ilipangwa kwa ajili ya kutajwa na akaomba ipangiwe tarehe
nyingine ya kuitaja.
Hakimu
Simba ameahirisha hadi Novemba 30, 2017. Washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Mhariri wa gazeti la Mawio, Simon Mkina,
Jabir Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehboob.
Lissu
na wenzake Simon Mkina, Jabir Idrisa na
Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehbooh wanakabiliwa na mashtaka
matano ikiwamo la kuandika habari za uchochezi kinyume na Sheria ya Magazeti ya
Mwaka 2002.
Inadaiwa
kuwa Januari 12 hadi 14, 2016 katika jiji la Dar es Salaam, washtakiwa watatu,
Jabir, Mkina na Lissu, kwa pamoja waliandika na kuchapisha taarifa za
uchochezi zenye kichwa cha habari kisemacho, ‘Machafuko yaja Zanzibar’.
Katika
shtaka la pili wanadaiwa kuwa Januari 14, 2016 katika jiji la Dar es Salaam,
walichapisha habari hizo ili kuleta chuki kwa wananchi wa Zanzibar.
Mshtakiwa Mehboob
anadaiwa kuwa Januari 13,2016 katika jengo la Jamana lililopo Manispaa ya
Ilala, Dar es Salaam, alichapisha gazeti
la Mawio lililokua na taarifa za uchochezi.
Alidai mshtakiwa huyo
pia alichapisha gazeti hilo bila ya kuwasilisha
hati ya sheria ya kiapo kwa Msajili wa
Magazeti.
Mbali na mashtaka
hayo washtakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kuwa Januari 14, 2016, Dar es Salaam,
bila ya kuwa na mamlaka yoyote, waliwatisha na kuwatia hofu wananchi wa
Zanzibar wasiweze kuingia kwenye
marudio ya Uchaguzi Mkuu.
No comments:
Post a Comment