Droo Kombe la Dunia 2018 kufanyika Disemba 1 Urusi...soma habari kamili na Matukio360...#share

Na mashirika ya kimataifa
BAADA ya mataifa 32 kufanikiwa kufuzu fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani nchini Urusi, droo ya kupanga makundi ya timu hizo itafanyika Ijumaa ya Desemba 1 mjini Moscow.

Kuelekea zoezi hilo baadhi ya timu ambazo zimepangwa kundi moja ni kundi la kwanza ambalo lina timu mwenyeji Urusi, Ujerumani, Brazil, Ureno, Ajentina, Ubelgiji, Poland na Ufaransa.

Afrika inawakilishwa na Misri, Nigeria, Morocco, Tunisia na Senegal.

Na kuelekea fainali hizo FIFA wamesema mpaka sasa kuna maombi milioni 3.5 ya tiketi na walioomba wengi wao ni wenyeji Urusi.

Makundi Kombe la Dunia yalivyopangwa
Kundi 1              Kundi  2            Kundi 3               Kundi 4
Urusi (wenyeji)  Uhispania (8)    Denmark (19)    Serbia (38)
Ujerumani (1)    Peru (10)          Iceland (21)       Nigeria (41)
Brazil (2)           Uswizi (11)        Costa Rica (22) Australia (43)
Ureno (3)          England (12)     Sweden (25)     Japan (44)
Argentina (4)     Colombia (13)   Tunisia (28)       Morocco (48)
Ubelgiji (5)        Mexico (16)      Misri (30)          Panama (49)
Poland (6)        Uruguay (17)     Senegal (32)     Korea Kusini (62)

Ufaransa (7)      Croatia (18)       Iran (34)            Saudi Arabia (63)

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search