Mugabe ateta na mkuu majeshi Zimbabwe...soma habari kamili na Matukio360..#share

Na mashirika ya kimataifa

WAKATI Jeshi nchini Zimbabwe linamzuilia rais Robert Mugabe nyumbani kwake katika mji mkuu wa nchi hiyo Harare amezungumza na mkuu wa majeshi wa nchi hiyo, Jen Constantino Chiwenga



Mkutano kati ya rais Robert Mugabe na mkuu wa majeshi ya Zimbabwe Jen Constantino Chiwenga pamoja na wajumbe kutoka Afrika Kusini katika ikulu ya rais Harare zimetolewa.

Mugabe ambaye hana mpango wa kujiuzulu kwa hiari alimwambia rais wa Afrika Kusini Jocub Zuma kwa njia ya simu kwamba yuko salama.

Hatua za kijeshi zilifuatia baada ya  kufutwa kwa Makamu wa Rais Emmerson Mnangagwa ambaye ni hasimu mkubwa wa wa mke wa Mugabe, Bi Grace Mugabe.

Hata hivyo kiongozi wa upinzani nchini humo Morgan Tsvangirai amemtaka Mugabe ajiuzulu wa hiari kabla ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwakani.

Wanajeshi wanashika doria katika barabara za Harare baada ya kuchukua udhibiti wa runinga ya taifa katika kile walichosema ni juhudi za kuwaandama "wahalifu".

Hatua hiyo huenda ikawa juhudi za kutaka kumuondoa madarakani Mugabe na badala yake kumuingiza madarakani makamu wake wa rais Emmerson Mnangagwa, ambaye alimfuta kazi wiki iliyopita.

Kufutwa kwa  Mnangagwa wiki iliyopita kulikuwa kumemuweka mke wa Rais Mugabe, Grace, katika nafasi nzuri ya kumrithi.

 Mugabe, 93, ameongoza taifa hilo tangu lilipojipatia uhuru mwaka 1980 kutoka kwa Uingereza.

Wanajeshi nchini Zimbabwe walichukua udhibiti wa kituo cha taifa cha utangazaji usiku na milipuko mikubwa ilisikika pamoja na ufyatuaji wa risasi usiku kucha mjini Harare.

Jenerali mmoja wa jeshi alitokea kwenye runinga na kusisitiza kwamba hakujatekelezwa mapinduzi ya kijeshi.

Alisema Rais Robert Mugabe na familia yake "wako salama salimini."

Lakini mzozo kuhusu ni nani anaweza kumrithi Mugabe kati ya Bi Grace Mugabe na Bwa Mnangagwa umekigawanya chama cha Zanu-PF miezi ya hivi karibuni.
Nchi za Jumuia ya maendeo ya kusini mwa Afrika (SADC) jana (Alhamisi) zilifanya  mkutano wa dharura nchini Botswana.

Umoja wa Afrika (AU) umesema  hatua ya jeshi la Zimbabwe ni kama mapinduzi

Siku ya Jumatano wanajeshi wakiwa na magari ya jeshi walilizinga bunge na majengo mengine makuu ya serikali.

Saa kadha baadaye walichukua udhibiti wa makao ya kituo cha habari cha serikali ZBC na kutangaza kuwa walikuwa wanawalenga waalifu wanamzunguka Rais Mugabe.

Hata hivyo meja Jenerali Sibusiso Moyo alikana kuwa hakukukuwa na mapinduzi wa kijeshi na kuwa Mugabe na familia yake walikuwa salama.



About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search