DSE: Thamani za hisa zapungua...soma habari kamili na Matukio360..#share
Na Hussein Ndubukile
SOKO la Hisa Dar es Salaam(DSE) limesema thamani ya mauzo
ya hisa imepungua kutoka bilioni 20 kwa wiki iliyoishia Oktoba 27 hadi bilioni 3 ya wiki iliyoishia Novemba 3 mwaka
huu.
Ofisa mwandamizi wa masoko wa Dar es Salaam wa DSE, Mary Kinabo
Hayo yamesemwa leo na
Ofisa Mwandamizi wa Masoko wa Dar es Salaam wa DSE, Mary Kinabo wakati
anawasilisha yaliyojiri kwenye soko hilo kwa wiki iliyoishia Novemba 3 mwaka
huu.
Amesema
idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa imepanda kutoka hisa milioni 1.6 ya wiki
iliyoishia Oktoba 27 hadi hisa milioni 3.5 ya wiki iliyoishia tarehe 3 mwezi
Novemba, 2017.
"
Kampuni zilizoongoza katika mauzo ya soko la hisa ni TCC (41%), Tanzania
Breweweries Ltd (27%), Benki ya CRDB
(16%) na VODA (11%), amesema.
Amebainisha
kuwa ukubwa wa mtaji wa kampuni zote zilizoorodheshwa katika soko umepungua kwa
Sh bilioni 217 kutoka Sh bilioni20.5 wiki iliyopita hadi Sh Trilioni 20.2 wiki
ilioyoishia Novemba 3 mwaka huu na kwamba punguzo hilo limetokana na kupungua
kwa bei za hisa za KA (8%), JHL (8%), CRDB (6%) na TBL (5%).
Amessisitiza
kuwa ukubwa wa mtaji wa kampuni za ndani umepungua kutoka Sh bilioni 112 kutoka
Trilioni 10.163 hadi kufikia Sh trilioni 10.051 wiki hii ikisababishwa na
kupungua kwa bei za hisa za kampuni za CRDB (6%) na TBL (5%).
Amefafanua
kuwa mauzo ya hati fungani katika wiki iliyoishia Novemba 3 yalikuwa Sh bilioni
15.7 kutoka Sh milioni 500 wiki iliyopita ya Oktoba 27 mwaka huu.
Ameongeza
kuwa mauzo hayo yametokana na hatifungani 11 za Serikali na za Makampuni
binafsi zenye jumla ya thamani ya Sh bilioni 15.7.
Pia
amesema kiashiria cha kampuni zote zilizoorodheshwa katika soko hilo yaani DSEI
kimeshuka kwa pointi 23 kutoka pointi 2,124 hadi 2,101 kutokana na kushuka kwa
bei za hisa za Shrika la Ndege la Kenya(KA) Jubilee Holdings ltd (JHL), CRDB na
TBL.
Katika
hatua nyingine, amesema kiashiria cha kampuni za ndani (TSI) kimepungua kwa
pointi 43 kutoka pointi 3,876 hadi 3,833 sababu ya kushuka kwa bei za hisa za
CRDB na TBL..
Wakati
huo huo, ameanisha kuwa kiashiria cha sekta ya viwanda kimepungua kwa poiti 77
kutoka pointi 5,379 hadi 5,303,
kiashiria cha huduma za kibenki na fedha kimeshuka kwa pointi 33 kutoka
pointi 2,497 hadi 2,464 huku cha Sekta ya huduma za kibiashara wiki hii
kimebaki kama awali kwenye wastani wa pointi 2,462.
No comments:
Post a Comment