Mkuu wa mkoa apiga marufuku kuzungumzia ukame...Soma habari kamili na Matukio360..#share
WAKAZI wa Mkoa wa Dodoma wamepigwa marufuku kuzuangumzia suala
la ukame.
Mkuu wa Mkoa Dodoma Dk. Binilith Mahenge
Pia amewataka watumishi kuwapa elimu wakulima ili walime mazao
yanayostahimili ukame.
Marufuku hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa huo Dk. Binilith
Mahenge alipokuwa akizungumza na watumishi wa wilaya ya Chemba, amesema mkoa huo unafaa kilimo cha mazao mengi.
“Kutamka ukame ni kisingizio cha uvivu na ni sawa na watu
wasiokuwa na maono, mkoa huu unafaa katika kilimo cha mazao mengi ,” amesema
Dk. Mahenge.
Aidha amewaagiza wakuu wa wilaya kuhakikisha wanashughulikia matatizo
mengine lakini isiwe katika suala la njaa.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga amesema wilaya yake
imeweka mikakati ya kujitosheleza kwa chakula na kumaliza migogoro ambayo
hupunguza muda wa uzalishaji.
Odunga amesema Chemba imejidhatiti kupambana na upungufu wa
chakula na wanayo ardhi ya kutosha kwa ajili ya kilimo.
"Hata hivyo tumeainisha mazao yanayotakiwa kulimwa kwa kila
kata kutokana na mtawanyiko wa mvua za msimu," amesema Odunga.
Hata hivyo mkuu huyo amesema kuwa tofauti na maeneo mengine,
Chemba wameendelea kukaribisha mifugo kwa kuwa ndiyo fursa kwao katika
kuchangia maendeleo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Rehema Madenge amesema mambo
mengi yatafanikiwa ikiwa watumishi watafuata utaratibu na kutimiza wajibu wao.
Kwa mujibu wa Madenge bila ya kufuata utaratibu mzuri wa
kiusimamizi hakuna kinachoweza kubadilika mkoani humo.
No comments:
Post a Comment