Hukumu kesi mtoto wa Chacha Wangwe Novemba 15...soma habari kamili na Matukio360..#share
Na
Abdulrahim Sadiki
HUKUMU
ya kesi ya kuchapisha taarifa za uongo kwenye mtandao wa kijamii inayomkabili, BOB Chacha Wangwe ambaye ni mtoto wa
mwanasiasa marehemu ,Chacha Wangwe, itatolewa Novemba 15, 2017
Hukumu
hiyo inatarajiwa kutolewa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi siku hiyo baada ya upande wa Mashtaka kuwaita mashahidi
sita kutoa ushahidi kwenye kesi hiyo na mshtakiwa huyo kujitetea mwenyewe.
Kwa
mujibu wa kesi hiyo namba 167, 2016
ambayo ilifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Mei 12,2016. Bob Chacha Wangwe ambaye kitaaluma ni mwanasheria na
mwanaharakati wa haki za binadamu anadaiwa kutenda kosa la
kuchapisha taarifa za kupotosha katika ukurasa wake wa Facebook.
No comments:
Post a Comment