Hukumu kesi ya Lulu dhidi Kanumba leo...soma habari kamili na Matukio360..#share

Na Abdulrahim Sadiki
LEO Novemba 13, 2017 Mahakama Kuu ya Tanzania inatarajia kutoa hukumu ya kesi ya kuuwa bila kukusudia inayomkabili Elizabeth Michael 'Lulu'

Masnii wa filamu, Elizabeth Michael 'Lulu'
Hatua hiyo itafuatia baada ya  wazee watatu wa Baraza kutoa ushauri wao kwa mahakama kwamba Lulu' ameua bila kukusudia au la.

Lulu anakabiliwa na kesi ya kuuwa bila kukusudia, akidaiwa kumuuwa msanii mwenzake, Steven Kanumba April 7, 2012.

Awali kabla ya wazee kutoa maoni hayo, Jaji Sam Rumanyika alisoma maelezo ya ushahidi wa pande zote mbili kisha kusikiliza maoni hayo.

Kabla ya kutoa maoni hayo, Jaji Rumanyika alisema kimsingi ushahidi wa upande wa mashtaka umejikita kwenye ushahidi wa kimazingira kwa sababu Lulu ndiye mtu wa mwisho kuwa na Kanumba.

Alisema ushahidi wa kimazingira unakuwa sio wa moja kwa moja, licha ya kuwa una vipande mithili ya nyololo ambavyo vimeshikana.

"Hivyo waungwana mkumbuke katika utoaji wa maoni yenu sio lazima mthibitishe makosa, pia kama mkiona mshtakiwa hausiki basi msisite kuieleza mahakama,".

Akitoa maoni yake, Mzee wa Baraza Omary Panzi amesema Lulu ameua bila kukusudia.

Amesema kuwa hatua hiyo inatokana na ushahidi wa mdogo wake Kanumba, Seth Bosco ambaye alielezea ugomvi uliotokea baina ya Lulu na marehemu.

"Maoni yangu ni kwamba marehemu alikufa kwa sababu ya kuteleza ikizingatiwa ilikuwa ni usiku na kulikuwa na giza, na chanzo cha kutekeleza ni ugomvi wake na Lulu,".

Pia Mzee wa pili, Bi.Sarah  amesema Kanumba alikufa kutokana na ugomvi ambapo ushahidi pia umetueleza kulikuwa na giza.

" Hivyo Lulu hakuuwa makusudi bali aliuwa bila kukusudia, ".

Naye Mzee wa Tatu, Rajabu Mlawa ametoa maoni yake alisema kutokana na sababu zilizosomwa anaridhika na hakuna ubishi kuwa Lulu ana kosa la kuuwa bila kukusudia.

" Ameuwa bila kukusudia na nimeridhika na kilichosemwa, kwani Kanumba alikuwa na mwili mkubwa na alikuwa katika hali ya kulewa, hivyo inaonekana katika heka heka za ugomvi inawezekana Lulu alitumia nguvu kidogo ya kumsukuma Kanumba hadi kudondoka,".

Baada ya kutoa maoni hayo, Jaji Rumanyika alisema kuwa anatarajia kutoa hukumu ya kesi hiyo leo Novemba 13/2017.

     




About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search