IGP Sirro ataka ushindi Polisi Tanzania FC.. soma habari kamili na matukio360.. #share

Na mwandishi wetu
MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amewataka wachezaji wa timu ya Polisi Tanzania kujituma kwa bidii ili kuhakikisha wanafanya vizuri katika michezo iliyobaki ya Ligi daraja la kwanza kundi B ili kujihakikishia nafasi ya kucheza Ligi kuu msimu ujao.
Kikosi cha Polisi Tz FC kikiendelea kujifua 

IGP Sirro ameyasema hayo  Mkoani Kilimanjaro alipokuwa akizungumza na Viongozi na wachezaji wa timu hiyo katika kambi yao iliyopo Chuo cha Polisi Moshi.

Amesema iwapo wachezaji watajituma na kucheza kwa morali pamoja na kufuata maelekezo ya walimu wao itakuwa rahisi kupata mafanikio ambayo yanatarajiwa katika kipindi hiki ambacho michezo ndani ya Jeshi la Polisi imepewa kipaumbele kwa kuwa inasaidia kujenga Afya za Askari, Ukakamavu pamoja na kuboresha mahusiano baina ya Polisi na jamii.

"Hakikisheni mnapata ushindi na mimi pamoja na makamanda wengine tutawapa ushirikiano w a kutosha ili mwakani tuwaone Ligi kuu" Amesema Sirro.

Akizungumzia ujio wa IGP Sirro kuzungumza na timu hiyo Afisa Habari na Mawasiliano wa timu Frank Geofray amesema kitendo hicho kimeongeza hamasa na ndio maana wameibuka na ushindi wa goli 2 kwa 0 dhidi ya JKT Mlale.

Amesema baada ya wachezaji kuzungumza na IGP Sirro walipata hamasa kubwa na hivyo kucheza kwa morali na hivyo kupata alama tatu ambazo zimewafanya kufikisha Points 13 katika michezo 8.

Magoli ya Polisi yalifungwa na mshambuliaji hatari Patrick Athanas pamoja na mkongwe  Bantu Admin ambapo Polisi walionyesha kiwango kikubwa kwa muda wote wa mchezo huo.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search