Jalada kesi ya Aveva na Kaburu lalejeshwa Takukuru..soma habari kamili na Matukio360..#Share
Na
Abdulrahim Sadiki
JALADA la kesi inayowakabili viongozi wa klabu ya Simba, rais
Evans Aveva na makamo wake Godfrey Nyage
‘Kaburu’ limerejeshwa Takukuru. Kwa muda mrefu sasa lilikuwepo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).
Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva wa mbele akiwa na Makamu wake, Godfrey Nyage'Kaburu' wakiingia katika moja ya chumba cha mahakama ya hakimu mkazi kisutu
Hayo yamesemwa leo mbele ya
Hakimu Mkazi Mwandamizi, Mwambapa na Mwendesha Mashtaka wa Takukuru,
Leonard Swai.
Swai amedai jalada hilo limerudishwa juzi Takukuru kutoka kwa DPP na ametoa
maelezo ya kukamilisha zaidi upelelezi.
Hayo yameelezwa na
Swai, baada ya Wakili wa Utetezi
Philemon Mutakyawa kuuliza juu ya jalada
hilo lililokuwepo kwa DPP limefikia wapi.
Aveva na makamu wake
wanakabiliwa na Mashtaka matano ya
uhujumu uchumi.
Ikiwamo ya kughushi,
kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha wa Dola za Marekani (USD) 300,000.
No comments:
Post a Comment