TFF yatangaza kocha mpya Kilimanjaro Star, kutangaza kikosi chake kipya..soma habari kamili na Matukio360..#share
Na
mwandishi wetu
SHIRIKISHO
la mpira wa miguu nchini(TFF) limemtangaza kocha mpya wa timu ya soka ya
Kilimanjaro Star itakayoshiriki mashindano ya Chaleji nchini Kenya.
Msemaji wa TFF, Alfred Lucas
Leo
jijini Dar es Salaam afisa habari wa TFF, Alfred Lucas amemtangaza kocha huyo
kuwa ni Ami koradi Minje ambaye atahusika na mashindano ya Chaleji tu.
‘Kocha
huyu atahusika katika mashindano ya Chalenji tu, baada ya mashindano hayo
kuisha timu itarudi kwa kocha mkuu, Salum Mayanga
,’’
amesema
Akizungumza
katika utambulisho huo, Ami Minje amesema kesho atakitangza kikosi chake
kitakachoshiriki mashindano hayo ambayo Kilimanjaro Star ipo kundi moja na
wenzao wa Zanzibar Herroes.
‘Ningependa
niulizwe maswali zaidi kesho(Novemba 18,2017) mara baada ya kutangaza kikosi cha Kilimanjaro
Star kitakachoshiriki mashindano ya Chalenji
nchini Kenya,’’ amesema Minje
Hata
hivyo amesema amekuwa akifundisha soka
nchini Uingereza kwa takribani miaka 13 na kwamba alikuwa akirejea nchini
kusaidiana na kocha mkuu wa Taifa Star, Salum Mayanga
‘Nimekuwa
nikifundisha soka katika chuo cha michezo ch Hall College cha Uingereza na nina beji ya ufundishaji ya shirikisho
la soka duniani (FIFA),’’ amesema
Mashindano
hayo ya Chalenji ya mwaka 2017
yanayoandaliwa na baraza la soka afrika mashariki( CECAFA) yatafanyika Kenya.
No comments:
Post a Comment