Taasisi ya JK yafanya upasuaji wa kwanza kuzibua mishipa ya moyo.. soma habari kamili na Matukio360.. #share

 Na mwandishi wetu
 ya wagonjwa 20 wamefanyiwa upasuaji wa kuzibua mishipa ya moyo kupitia mshipa wa damu wa mkono (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cathlab hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa upasuaji wa aina hiyo kufanyika nchini.

Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Taasisi ya Kimataifa ya Kiislamu ya  Misaada (IIRO) ya nchini Saud Arabia wakimfanyia mgonjwa upasuaji
Akiongea na Waandishi wa Habari leo jijini Dar Salaam Daktari bingwa wa magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge amesema upasuaji huo unafanyika  katika kambi ya matibabu ya Moyo inayofanywa na Taasisi hiyo kwa kushirikiana na madakatari kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Kiislamu ya  Misaada (IIRO) ya nchini Saudi  Arabia.

Dkt. Kisenge amesema kuwa kambi hiyo inaenda sambamba na utoaji wa elimu na kubadilishana ujuzi wa kazi  kati ya wafanyakazi wa Taasisi hizo mbili ikiwemo aina mpya ya upasuaji wanaoufanya kitu ambacho kinawajengea uwezo zaidi. ”

“Faida ya upasuaji huu ni kumwezesha mgonjwa kutoka chumba cha upasuaji akiwa anatembea na baada ya masaa manne kama hali yake inaendelea vizuri anaweza kuruhusiwa.

 “Tofauti na upasuaji wa kutumia mshipa wa paja ambao tulikuwa tunaufanya, baada ya upasuaji mgonjwa ni lazima akae Hospitali kwa zaidi ya masaa 24 ili kuangalia maendeleo ya afya yake”, amesema Dkt. Kisenge.

Kwa upande wake  Daktari bingwa wa magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya IIRO Ali Al Masoud   amesema kambi hiyo inaendelea vizuri kwani kwa siku wanatibu wagonjwa 10 na baada ya matibabu afya zao zinaimarika tofauti na ilivyokuwa  kabla ya matibabu.

Dkt. Masoud aliongeza kuwa wamekuja na utaalam mpya wakuzibua mishipa ya moyo kupitia mshipa wa damu wa mkono ambapo kabla ya hapo matibabu yaliyokuwa yanafanyika ni ya kutumia mshipa wa damu wa kwenye paja.

Alifafanua, “Hivi sasa tunafanya upasuaji wa Moyo wa bila kufungua kifua  kitu ambacho wenzetu hawa walikuwa wanakifanya. Sisi tumewaongeza utaalam mpya wa kutumia  mshipa ya mkononi badala ya mshipa wa paja.

Naye Bader Alanezi ambaye ni Mtaalamu wa magonjwa ya Moyo na mishipa ya damu kutoka IIRO alimalizia kwa kusema kuwa  wamepata muda wa kujifunza vitu vingi na kupata uzoefu mpya  wa baadhi ya magonjwa na mambo ya kiteknolojia ambayo katika nchi yao hakuna.
Zoezi la kumfanyia mgonjwa upasuaji wa kuzibua mishipa ya moyo kupitia mshipa wa damu wa mkono (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cathlab likiendelea.
Jumla ya wagonjwa  40 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji katika kambi hiyo ya siku tano ambayo imeanza tarehe 14 hadi tarehe 18 mwezi huu.
Jopo la madaktari bingwa likiendelea na upasuaji.

Na Mwandishi wetu,

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search