Kigogo wa Takukuru apandishwa kizimbani...soma habari kamili na Matukio360..#share
Na
Abdulrahim Sadiki
ALIYEKUWA Mhasibu wa Takukuru, Godfrey Gugai amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu na wenzake watatu wakikabiliwa na mashtaka 43 likiwamo la kumiliki mali
ambazo hazina maelezo zenye thamani
bilioni 3.6 na utakatishaji wa fedha.
Akisoma
hati ya mashtaka leo kwa Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba, Wakili wa Serikali,
Wankyo Simon aliwataja washtakiwa wengine kuwa ni George Makaranga, Leonard
Alloys na Yasini Katera.
Washtakiwa
hao wanakabiliwa na shtaka moja la kumiliki mali ambazo hazina maelezo,
kughushi 22 na 20 ya utakatishaji wa fedha.
Amedai
kuwa kati ya Januari 2005 na Disemba 2015 Dar es Salaam Godfrey akiwa mtumishi
wa Umma aliyeajiliwa na Takukuru alikuwa na mali ambazo hazina maelezo zenye
thamani ya Sh 3,634,961,105.03 ambazo haziendani na kipato chake cha sasa na
cha nyuma ambacho ni Sh 852,183,160.46.
Imedaiwa
kuwa mshtakiwa huyo alipotakiwa kutoa maelezo ambayo yanaridhisha kuhusiana na
yeye kumiliki mali hizo, alishindwa kutoa.
Wankyo
amedai kati ya Januari na Juni, 2016 Dar
es Salaam, Gugai akishirikiana na
wenzake walighushi mikataba ya mauziano akionesha ameuza Mali zake kwa wenzake
na watu wengine wakati akijua siyo kweli.
Gugai
anadaiwa kuwa Agosti 14, 2009 alighushi
mkataba wa mauziano akionesha kuwa alimuuzia Zena Mgallah plot namba 225 block 6 Mbweni JKT, wakati akijua si kweli.
Amedai
kuwa Julai 5,2011 alighushi akionyesha
kumuuzia Salehe Sas plot namba 621,622 na 623 block A vilivyopo Gomba
Arumeru.
Oktoba
20,2013 alighushi akionesha alimuuzia Arif
Premji plot namba 64 kilichopo Onunio
Kinondoni.
Desemba 20, 2014 alighushi akionesha alimuuzia Edith Mbatia
plot namba 737 block C kilichopo Mwambani Mwarongo Tanga plot namba 1,2 na 3.
Gugai na George Novemba 20,2009 walighushi wakionesha Gugai
alimuuzia George plot namba 150 block 8 kilichopo Bunju Kinondoni.
Gugai na Leonard
wanadaiwa kuwa Novemba 19 ,2009, Gugai walighushi wakionesha alimuuzia Leonard
plot namba 275,277,296 na 297 block 2 zilizopo Nyamongo, Mwanza.
Washtakiwa hao,Gugai
na Leonard Agosti 20,2010 Gugai walighushi wakionesha alimuuzia Leonard plot
namba 90 block5 Bugarika Kwanza.
Wanaendelea
kudaiwa Septemba 10,2013 walighushi
wakionesha Gugai alimuuzia Leonard plot
namba 713 block B Kiseke Mwanza na
Oktoba 20,2015 akionesha kumuuzia plot namba 230.
Gugai Novemba 30,2011
wanadaiwa kughushi hati ya makubaliano ya umiliki wa kiwanja akionesha kumuuzia Manwali Masalakulangwa plot namba 14
block J Bunju na Novemba 15,2015 plot namba 103 na 104 Block L Bagamoyo.
Gugai Novemba 19,2015
wanadaiwa kughushi akionesha alimuuzia Masalakulangwa plot namba 184 block B
Buyuni Temeke na Novemba 4, 2011 akionesha kumuuzia Rose Abdallah plot namba 34
block K , B Centre Dodoma.
Iliendelea kudaiwa
kuwa Desemba 5,2013 alighushi akionesha
kumuuzia Rose Abdallah plot namba 32 block N, Itega Dodoma, Novemba 14, 2014
plot namba 47 block B kilichopo Mwongozo Temeke
na Novemba 30,2014 plot namba 24 na 39 block B na M vilivyopo Chidachi
na Itega Dodoma.
Gugai Septemba 2015
anadaiwa kughushi akionesha alimuuzia Patrick Magesa plot namba 7/9 na 11/13
block C vilivyopo Mwakidila Magaoni Tanga, Oktoba 15,2015 plot namba 18 block J
Mwarongo Tanga.
Iliendelea kudaiwa
kuwa Gugai anadaiwa kughushi akionesha Desemba 22,2015 alimuuzia Yasin Katera
plot namba 438 block D kilichopo Nyegezi Mwanza.
Desemba 22,2015 Gugai
anadaiwa kumuuzia Yasini Katera plot namba 439 block D Nyegezi Mwanza.
Kuanzia shtaka la 23
hadi 43 washtakiwa hao wakabiliwa na
Mashtaka ya utakatishaji wa fedha.
Anadaiwa kuwa kati ya
Januari na Juni, 2016 Dar es Salaam kwa njia ya udanganyifu kwa lengo la
kuficha umiliki wa Mali hizo kwa kuonesha zinamilikiwa na watu tofauti tofauti
wakati akijua si kweli na ni mazao ya Rushwa ambayo yametokana na kosa la kumiliki Mali bila maelezo.
Baada ya washtakiwa
hao kusomewa mashtaka hayo waliyakana na Wankyo alidai kuwa upelelezi bado
haujakamilika na kwamba tarehe ijayo wataeleza hali ya upelelezi.
Baada ya kueleza
hayo,
wakili Alex Mgongolwa akishirikiana na
wakili Semi Malimi walidai kuwa wamejiridhisha shtaka la 23 hadi 43 ya
utakatishaji wa fedha hayakidhi vigezo
vinavyotakiwa kwa makosa ya utakatishaji wa fedha.
Mgongolwa alidai kwa
kuwa makosa hayo ya utakatishaji fedha hayaelezi kosa husika hats kidogo
aliomba mahakama iyafutilie mbali chini ya kifungu cha 129 cha makosa ya Jinai
ama mahakama nitumie mamlaka yake ya asili kuyafuta.
Kwa kuwa ili liwe
kosa la utakatishaji fedha ni lazima kuwepo na kosa tangulizi, limefanyika na
kupelekwa kupatikana kwa fedha, unachukua fedha hizo ama kujengea na
ukauza kuanzisha kitu kingine.
Mgongolwa alidai kuwa
katika Mashtaka yanayowakabili wateja wake hayazungumzii fedha na fedha ndiyo
msingi wa shtaka la utakatishaji fedha na kwamba katika kesi hiyo
kinachojitokeza ni alidanganya Mali ya Fulani wakati siyo.
Mashtaka hayo hayana
kabisa uhusiano na utakatishaji wa fedha na kwamba makosa hayo hayana dhamana
ni lazima umakini katika tafsiri yake uwe wa hali ya juu.
Kwa mapungufu hayo
shtaka la 23 hadi la 43 hayana nafasi ya kusimama mbele ya mahakama yafutiliwe
mbali.
No comments:
Post a Comment