Miili 11 waliokufa ajali ya Ndege yapatikana...soma habari kamili na matukio
Na Mwandishi Wetu
MIILI ya watu 11 waliofariki katika ajali ya Ndege ya Shirika la Coastal
Aviation iliyoanguka jana eneo Empakai
Ngorongoro mkoani Arusha imepatikana leo.
Ndege hiyo ilianguka baada ya kugonga mlima majira ya sasa saba mchana
kutokana na matatizo ya hali ya hewa.
Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Theresia Mahongo amesema zoezi la kutafuta
miili limekwenda vizuri.
"Miili yote imepatikana na tutaipeleka Karatu na baadaye Arusha," amesema.
"Miili yote imepatikana na tutaipeleka Karatu na baadaye Arusha," amesema.
Naibu Mhifadhi wa hifadhi ya Ngorongoro, Dk Maurus Msuha amesema
wamefanikiwa kuipata miili na kuitoa eneo la ajali kutokana na ushirikiano
mkubwa na wenyeji.
"Tuliwaomba kulala hapa wenyeji jana kuilinda isiliwe na wanyama na
hadi leo tumeikuta miili salama," amesema.
Mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo, Lunda Mollel amesema ndege hiyo kabla
ya kuanguka ilikuwa inazunguka kutoka eneo la milima zaidi ya dakika 20 hadi
baadaye kuanguka baada ya kugonga mlima.
No comments:
Post a Comment