JUKATA kumfungulia kesi mwanasheria mkuu wa serikali..soma habari kamili na Matukio360..#share

Na Salha Mohamed
JUKWAA la Katiba
Tanzania (JUKATA), linatarajia kumfungulia kesi Mwanasheri Mkuu wa Serikali (AG) likidai kuminywa
na kuzuiwa na Jeshi la Polisi kufanya maandamano ya amani Oktoba 30, 2017.
Mwenyekiti wa Jukwaa la katiba Tanzania (JUKATA), Hebron Mwakagenda (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo na kutoa maamuzi ya Jukwaa baada y kukataliwa kufanya Maandamano ya amani Oktoba 30, 2017. Kushoto ni Msafiri Shabani Mjumbe na Marganius Msambila ambaye pia na mjumbe.
Maandamano
hayo yalilenga kuunga mkono jitihadi za rais John Magufuli katika
kusimamia rasilimali za taifa pamoja na kupiga vita rushwa.
Mwenyekiti
wa Jukwaa hilo, Hebron Mwakagenda leo jijini Dar es salaam amesema hawajapokea
barua ya kukubaliwa kufanya maandamano hayo kutoka Ikulu na walipokea barua
kutoka jeshi la Polisi kanda Maalum likiwakataza
kufanya maandamano.
"Tumefanya
uchambuzi wa sababu zilizotolewa na kuridhika kwamba ipo haja ya kuchukua hatua
zaidi.... Jeshi la Polisi liliainisha sababu tatu, "amesema.
Amesema
sababu hizo ni rais kutothibitisha kushiriki kwenye maandamano, kufanya maandamano
ya umbali mrefu kwa kufunga barabara
kutaathiri shughuli na Oktoba 30,2017 wanafunzi wa kidato cha nne
wanafanya mitihani.
"Kwasababu
hizi zilizotumika JUKATA tumefikia maamuzi ya kwenda kufungua kesi mahakamani
kudai haki ambayo inaminywa na kukandamizwa na Jeshi la Polisi kwa kutumia sababu
nyepesi, "amesema.
Amesema
wapo kwenye hatua za mwisho kutekeleza
uamuzi huo na kwamba jopo la mawakili wasiopungua kumi wakiongozwa na Dk.
Rugemeleza Nshala watahusika katika mchakato huo.
Mwakagenda
amesema miongoni ma sababu zinazosababisha kwenda mahakamani ni kuomba tafsiri
ya mahakama kuhusu namna jeshi la Polisi linavyotumia kifungu 43(3) na 44 ya
sheria ya Jeshi la Polisi ya mwaka 2002.
"Kwa
mtazamo wa uchambuzi wetu Jeshi la Polisi limekuwa likitumia vibaya vifungu hivi
kuzuia mikutano pamoja na maandamano ya amani kinyume na uhalisia wa vifungu
hivi kwa kisingizio cha uwepo wa taarifa za kiintelijensia kuwa kuna viashiria
vya uvunjifu wa amani, "amesema.
Akizungumzia
suala la katiba mpya, Mwakagenda amesema
jukwaa hilo linaendelea kusisitiza haja na umuhimu wa kukamilishwa kwa mchakato
huo.
Amesema
imethibitika kuwa asilimia 67 ya wananchi wanaona ni muhimu Tanzania kupata
katiba mpya.
"
Ni muhimu serikali kutekeleza jambo hili kwakuwa pia lipo kwenye ilani ya
uchaguzi ya chama tawala, CCM. "...tunasisitiza serikali kufanya marekebisho
kwenye katiba ya sasa endapo mchakato wa katika haujakamilika 2020 wakati a uchaguzi ili kuondoa dosari ambazo
zimekuwa zikilalamikiwa kila uchaguzi, "amesema.
No comments:
Post a Comment