Mchoro wa Yesu wauzwa dola milioni 450....soma habari kamili na Matukio360..#share
Na mashirika ya
kimataifa
MCHORO wa miaka 500
wa Yesu unaoaminiwa kuchorwa na Leonardo da Vinci, umeuzwa mjini New York kwa
dola milioni 450.
Mchoro wa Yesu Salvator Mundi au (Mkombozi wa Dunia) umeuzwa dola
milioni 450 Marekani
Mchoro huo
unajulikana kama Salvator Mundi (Mkombozi wa Dunia). Ndio mchoro wa bei ya juu
zaidi kuwai kuuzwa kwa mnada.
Hata hivyo Simu ya Hitler iliuzwa dola 243,000 Marekani. Leonardo da Vinci aliyefarika
mwaka 1519 ana michoro 20 iliyobaki.
Ni huo mmoja tu
unaoaminiwa kuwa mikononi mwa mtu ambao unaamimiwa kuwa ulichorwa baada ya
mwaka 1505.
Picha hiyo
inamuonyesh Yesu akiwa ameinua mkono mmoja huku mwingine ukishika kioo.
Mwaka 1958 mchoro huo
uliuzwa kwenye soko la mnada mjini London kwa Dola 60. Wakati huo mchoro huo
uliaminiwa kuwa kazi ya mfuasi wa Leonardo na wala haukuwa wa Leonardo
mwenyewe.
Miaka
minne iliyopita mchoro huo ulinunuliwa na raia wa Urusi kwa dola milion 127.5
lakini wakati huo hakuuzwa katika mnada.
No comments:
Post a Comment