Kesi kigogo TRA anayemiliki gari 19 kuunguruma... soma habari kamili na Matukio360..#share
Na Abdulrahim Sadiki
AfFISA Msaidizi wa
Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Jennifer Mushi anayekabiliwa na
mashtaka mawili ikiwamo la kukutwa akimiliki magari 19, mali isiyolingana na kipato chake halali
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, atasomewa maelezo ya awali Desemba 6,
2017.
Jennifer ameshtakiwa
chini ya kifungu cha 27, (1) (a) na (b) cha sheria ya kuzuia na kupambana na
rushwa namba 11ya mwaka 2007.
Alipaswa kusomewa
maelezo hayo ya awali leo lakini Wakili wa Serikali Mkuu, Vitalis Peter
ameieleza mahakama kuwa bado hawajamaliza kuandaa maelezo.
Hakimu Shaidi ameaihirisha
kesi hiyo hadi Desemba 6,2017 ambapo mshtakiwa huyo atasomewa maelezo hayo ya
awali (PH).
Mshtakiwa huyo anayetetewa
na wakili Elisaria Mosha anadaiwa kuwa
kati ya Machi 21,2016 na Juni 30,2016
jijini Dar es Salaam akiwa mwajiriwa wa TRA kama Afisa Forodha Msaidizi
alikutwa akimili magari 19.
Magari hayo ni Toyota
Dyna Truck, Toyota Vizt, Toyota RAV4, Suzuki
Carry, Toyota Ipsum, Toyota Wish, Toyota Mark II, Toyota Wish na Toyota Mark X.
Mengine ni Toyota
Estima Toyota Regiusage, Toyota Estimated, Toyota Alex, Toyota Noah, Toyota
Crown, Toyota Hiace, , Toyota Passo na
Suzuki Carry yote yakiwa na thamani ya Sh 197,601,207 Mali ambayo hailingani na
kipato chake halali.
Anadaiwa
kuwa, kati ya Machi 21 ,2012 na Machi 30,2016 Dares Salaam akiwa mwajiriwa wa
TRA kama Afisa Forodha Msaidizi alikutwa akiishi maisha ya kifahari yenye thamani ya Sh 333,255,556.24 fedha
ambayo hailingani na Kipato chake halali.
Baada
ya kusomewa mashtaka hayo mshtakiwa huyo alikana na yupo nje kwa dhamana.
No comments:
Post a Comment