Polisi wakamata simu ya Zitto, kupekua ofisi ACT...soma habari kamili na Matukio360..#share
Na mwandishi wetu
JESHI la Polisi limeikamata simu ya kiongozi
mkuu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe na litapekua ofisi ya makau makuu ya chama
hicho.
Zitto Kabwe
Katibu - Itikadi, Uenezi na Mawasiliano ya
Umma wa ACT, Ado Shaibu leo ameiambia Matukio360 kuwa Zitto aliripoti
kituo cha Polisi Kamata jijini Dar es salaam kama alivyotakiwa awali na jeshi
hilo.
‘Jeshi la Polisi limechukua simu ya ndugu
Zitto kwa maelezo kuwa itasaidia uchunguzi wao, na wameahidi kuwa watairudisha
kwake kesho jioni, na ametakiwa kurudi kituoni hapo Novemba 21, 2017,’ amesema
Shaibu
‘Pia Jeshi la Polisi limetoa
taarifa kuwa litakwenda katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama cha ACT Wazalendo,
kwa Lengo la kufanya upekuzi wa Ofisi hizo wakitafuta nyaraka zilizotumika na
Chama kufanya Uchambuzi wa Takwimu za Serikali ambao unaonyesha Uchumi wa Nchi
yetu "UNASINYAA".
No comments:
Post a Comment