Makalla apiga marufuku ununuzi wa migomba shambani..soma habari kamili na Matukio360..#share
Na mwandishi wetu
MKUU wa mkoa wa
Mbeya, Amos Makalla amepiga marufuku ununuzi wa migomba ikiwa shambani kwa kuwa
inapunguza kipato kwa wakulima.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla kulia akizungumza na mfanyabishara wa ndizi Sophia Mwakyusa kushoto alipotembelea katika soko la muda la Kiwira Wilayani Rungwe mkoani Mbeya .
Pia amesema ujenzi wa
soko la kimataifa la zao la ndizi
unatarajiwa kujengwa mwakani na eneo limepatikana.
Amesema hayo
alipokuwa akijibu hoja zilizotolewa na wakulima wa zao hilo wilayani Rungwe na
kwamba wafanyabiashara wanapaswa kununua mkungu wa ndizi uliokomaa.
“Pamoja na mambo mengine nataka
wafanyabiashara kuacha tabia ya
kununua ‘kuchumbia’ migomba shabani hii ni changamoto inayosababisha wakulima
kutonufaika na zao hilo. Wanunue mkungu wa ndizi uliokomaa na vinginevyo,” amesema
na kuongeza
“Miongoni mwa utekelezaji
wa vipaumbele ambayo tumejiwekea hapo mwakani ni ujenzi wa soko la kimataifa la zao la
ndizi, eneo linalokidhi vigezo kwa ajili
ya mradi huo limepatikana.”
Awali wakulima wa
ndizi waliitaka serikali kuharakisha
ujenzi wa soko hilo ili kufungua fursa
za kiuchumi na thamani ya zao hilo kutokana na kukosekana kwa soko la uhakika
Wakizungumza na kwa nyakati tofauti na Matukio 360 wamesema zao limeshuka thamani
kwa kiasi kikubwa hadi baadhi ya
wafanyabishara kununua kwa bei ambayo hailingani na gharama za uzalishaji.
Mkulima, Amos Joseph
amesema endapo serikali ikikamilisha
mradi huo kuna uwezekano mkubwa wa
mapato na uchumi wa wilaya ya Rungwe kukua.
"Ukosefu wa soko
la zao ndizi ni changamoto inayosababisha kuuza kwa bei ya hasara. Mkungu mmoja
tunauza kwa bei ya sh 2,000
hadi 4,000 kulingana
na ukubwa,"amesema.
Naye Sophia Mwaikambo
amesema pia halmashauri inapoteza mapato kutokana na kutokuwapo kwa soko la
uhakika la zao hilo
No comments:
Post a Comment