Kesi vigogo wa Tanesco kuunguruma Novemba...soma habari kamili na Matukio360...#share
Na
Abdulrahim Sadiki
KESI ya hujumu uchumi inayowakabili
vigogo watano wa zamani wa Shirika la umeme nchini(Tanesco) na msambazaji kutoka kampuni ya M/S Young Dong
Electronic Co. Ltd itaanza kuunguruma Novemba 30, 2017.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
Vigogo
hao ni mkurugenzi wa Fedha, Lusekelo Kasanga, naibu mkurugenzi mkuu wa Tanesco,
Robert Shemhilu, ofisa ugavi, Harun Mattambo,
mwanasheria wao, Godson Makia na msambazaji Martin Simba.
Wanashtakiwa kwa kuisababishia
Serikali hasara ya milioni 275. Kesi hiyo itaanza
kusikilizwa kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu, Thomas Simba.
Washtakiwa
hao wanakabiliwa na mashtaka mawili ya uhujumu uchumi ikiwamo matumizi mabaya ya
madaraka na kusababisha hasara milioni
275.Upande wa Mashtaka
unawakilishwa na Wakili Mkuu wa Serikali, Vital is Peter.
Wanadaiwa kati ya Januari na Desemba 2011 katika ofisi
za Tanesco Ubungo, washtakiwa hao
wakiwa waajiriwa wa shirika hilo,
walitumia madaraka yao vibaya kwa kufanikisha malipo kwa msambazaji Martin
Simba bila ya kufanya uhakiki.
Imedaiwa walifanya hivyo kinyume na kifungu cha 35 cha
Sheria ya Manunuzi ya Umma namba 21 ya
2014 kitendo ambacho kilisababisha msambazaji huyo kupata faida.
Imedaiwa kati ya Januari na Desemba, mwaka 2011 katika ofisi za Tanesco Ubungo,
washtakiwa hao wakiwa waajiriwa wa shirika hilo pamoja na msambazaji huyo
waliisababishia Serikali hasara ya Sh
275,040,000. Washtakiwa hao wapo nje kwa dhamana.
No comments:
Post a Comment