Kigogo wa Escrow aachiwa huru...soma habari kamili na Matukio360...#share
Na
Abdulrahim Sadiki
ALIYEKUWA
mkurugenzi wa huduma za sheria wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, Rugonzibwa Mujunangoma ameachiwa huru na mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
Alikuwa
akikabiliwa na shtaka la kupokea rushwa
ya milioni 323 kutoka kwa James Rugemalira fedha ambazo ni sehemu ya fedha za
Akaunti ya Tegeta Esrow.
Leo
Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa amemuachia huru Rugonzibwa baada ya
Mwendesha Mashtaka Mwandamizi wa Takukuru, Leonard Swai kuomba kesi hiyo
iondolewe mahakama chini ya kifungu cha 98 (a) cha sheria ya Makosa ya Jinai (CPA) na mahakama
kuridhia.
Rugonzibwa
alifikishwa mahakama kwa mara ya kwanza Januari 14,2015 na Taasisi ya Kuzuia na
Kupamba na Rushwa (Takukuru).
Akikabiliwa
na shtaka la kupokea rushwa ya milioni 323 toka kwa James Rugemalira fedha ambazo ni
sehemu ya fedha za Akaunti ya Tegeta Esrow.
Ambapo
baadaye alibadilishiwa hati ya Mashtaka na kusomewa upya ambapo hayakuonesha tena kuwa fedha
zilizopokelewa na Mujunangoma toka kwa Rugemalira ni sehemu ya fedha za Akaunti
ya Tegeta Escrow.
Kupitia
hati hiyo mpya, Rugonzibwa alikuwa
akidaiwa kuwa Februari 5, 2014 akiwa
mtumishi wa serikali kama Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alipokea rushwa ya milioni 323 kupitia akaunti
yake namba 00120102602001 iliyopo kwenye
benki ya Mkombozi .
Alidaiwa
kuwa alipokea kiasi hicho cha fedha kutoka kwa James Burchard Rugemalira,
ambaye ni mshauri huru wa kitaalamu, mkurugenzi wa VIP na mkurugenzi wa zamani
wa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL kama tuzo kwa kushughulikia mambo ya ufilisi
wa muda wa kampuni hiyo.
Iliendelea
kudaiwa kuwa baada ya kujipatia kiasi hicho cha fedha alishindwa kueleza
maslahi yake kwa Katibu Mkuu wa Wizara yake ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi na kwenye tume ya maadili ya
Viongozi.
Baada
ya kusomewa mashtaka hayo, alikana na upelelezi
wa kesi hiyo ulikuwa umekwisha
kamilika.
Awali Mujunangoma alikuwa akidaiwa kuwa Februari 5, 2014 katika Benki ya Mkombozi
iliyopo wilayani Ilala, Dar es Salaam, akiwa Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi alipokea rushwa ya kiasi hicho cha fedha kutoka kwa James
Burchard Rugemalira kama tuzo kwa
kushughulikia mambo ya ufilisi wa muda wa kampuni hiyo fedha ambazo ni sehemu
ya fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow.
Mshtakiwa
huyo anadaiwa kufanya kosa hilo, kinyume
na kifungu cha 15 (1)cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Namba 11 ya
mwaka 2007 na alikuwa yupo nje kwa dhamana.
No comments:
Post a Comment