Kigamboni yaongoza kitaifa...soma habari kamili na Matukio360...#share
Na
mwandishi wetu
HALMASHAURI
ya manispaa ya Kigamboni imeongoza kwa kuwa ya kwanza kitaifa kati ya
halmashauri 186 katika uwezeshaji wanawake nchini.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh. Selemani Jafo (Katikati) akizungumza na wafanyakazi
Hayo yamesemwa na Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, Seleman Jafo wakati akizungumza na maafisa maendeleo ya jamii kutoka katika halmashauri zote nchini.
Hivi karibuni halmashauri ya manispaa ya Kigamboni imeonekana kufanya vizuri katika mambo mbalimbali ikiwemo kuingia katika kumi bora matokeo ya mtihani wa darasa la saba, kushika namba moja kwa Mkoa wa Dar es salaam katika masuala ya afya nk.
Wachambuzi
wa mambo wanasema mafanikio hayo ya wilaya mpya nchini iliyoanza kufanya kazi
Disemba 2016 yametokana na ushirikiano mzuri wa utendaji kazi na uwajibikaji
uliopo miongoni mwa viongozi wa wilaya hiyo.
Mara
kwa mara mkuu wa wilaya hiyo, Hashim Mgandilwa na mkurugenzi wa manispaa ya
Kigamboni Stephen Katemba wameonekana wakiwa na ushirikiano thabiti ambao tija
yake imeonekana katika mafanikio wanayoyapata licha ya wilaya hiyo kuwa mpya.
Aidha,
balaza la madiwani, mbunge wa Jimbo la Kigamboni Mhe Dkt Faustine Ndungulile
pia wameonekana kushikamana kwa kuweka mipango na mikakati ya pamoja ambayo
imesaidia kupata mafanikio haya.
No comments:
Post a Comment