Polisi wamsaka aliyenyuma 'mnunuzi' nyumba Lugumi...Soma habari kamili na Matukio360..#share
Na Abraham Ntambara
JESH la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamtafuta
aliyemtuma Dk. Louis Shika (48) mkazi wa Tabata kuharibu mchakato wa uuzwaji wa
nyumba za mfanyabiashara Said Lugumi kwa njia ya mnada ili kuweza kumfikisha katika
vyombo vya sheria.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Hayo yamebainishwa leo na
Kamishna wa Polisi Kanda hiyo SACP Lazaro Mambosasa, akizungumza na waandishi
wa habari, amesema jeshi hilo linamhisi mfanyabiashara huyo ndiye aliyemtuma
kutokana na kudai kuwa fedha zitatoka Urusi huku ikijulikana kuwa Lugumi aamekimbia nchini.
“Tunachoendelea kufuatilia ni kujua ni nani aliyemuajiri akazuie
mnada kufanyika na kwa vyovyote vile ukitumia logic thinking ni kwamba mwenye
kula hasara kama zitauzwa ni yeye mmiliki wa nyumba ambaye kimsingi alikwisha
kimbia nchini,” amesema SACP Mambosasa
“Na huyu bwana kumbuka anasema fedha zinatoka Urusi na huyo
bwana alikojificha anajua mwenyewe
Sasa huko Urusi inawezekana ndiko huyu mhalifu mweingine ambaye
kimsingi anadaiwa na TRA, kwa hiyo kuna uhusiano, mtu yeyote mwenye busara yake
atajua kwa nini huyu mtu ameingilia kuzuia mnada huu,” ameongeza.
SACP Mambosasa amebainisha kuwa kwa sasa kwa upande wa Dk.
Shika, wanaendelea na hatua za upelelezi na pindi utakapokamilika jarada
litakwenda kwa mwanasheria kwa ajili ya uandaaji wa hati ya mashtaka kwa ili mhusika
kupelekwa mahakamani.
Tukio hilo lilitokea jana wakati wa mnada wa
uuzwaji wa nyumba za mfanyabiashara huyo, mtuhumiwa huyo alishinda mnada huo kwa
kutaka kununua nyumba zote tatu, nyumba moja ya Mbweni alitaka kununua kwa sh.
bilion 1,200,000,000, nyumba ya pili Mbweni alishinda na alitaka kununua kwa
sh. milioni 900,000,000 na nyumba ya tatu ya Upanga alishinda na kutaka kununua
kwa sh. bilioni 1,200,000,000.
Lakini alipotakiwa kulipa fedha taslimu asilimia 25 ya mnada kwa
kila nyumba, hakuwa na fedha ndipo alipokamatwa na jeshi hilo na kufukishwa
kituoni na upelelezi wa kesi hiyo
unaendelea na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.
Kwa upande mwingine SACP Mambosasa amesema wanamshikilia
Willliam Lugita Jeremia (56) akijinadi ni wakili wa kampuni ya Faithfull Attorney
Advocates huku akijua siyo wakili.
Amesema baada ya mahojiano mtuhumiwa amekiri kuwa si wakili ila aliwahi kusoma shahada ya sheria mwaka 2004 katika chuo Kikuu cha Dar
es Salaam na alikuwa mahakamani kuwakilisha wateja wake Nunu Muhamisy na
wenzake katika MISC Application namba 9/2017 iliyokuwa inasikilizwa na Jaji Mahuru.
Pia mtuhumiwa ameeleza kuwa aliwahi kufanya kazi katika Fame ya
Marando mwaka 2014 akiwa katika mafunzo ya vitendo na ameshawahi kusimamia kesi
nyingi akiwa kama wakili.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa jana akiwa katika Mahakama Kuu Kitengo
cha Ardhi Mtaa wa Kivukoni kufuatia kitendo hicho, upelelezi wa kesi hiyo
unaendelea na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za
kisheria.
No comments:
Post a Comment