MCT yaonya uvunjifu wa haki za wanahabari...soma habari kamili na Matukio360..#share
Na Abraham Ntambara
BARAZA la Habari Tanzania (MCT) limesema takribani matukio 30 yameonyesha uvunjifu wa uhuru wa habari nchini.Pia MCT itawafikisha mahakamani wote wanaowazuia, kuwanyanyasa na kuwapiga waandishi wa habari wawapo katika majukumu yao.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Kajubi Mukajanga (Kulia) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Maelezo hayo yametolewa leo jijini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji
wa MCT, Kajubi Mukajanga katika maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Kupinga
Jinai Dhidi ya Wanahabari, yanayofanyika duniani kote na kwamba baraza
linachukua hatua hiyo kutokana na vitendo hivyo kushamiri .
Akitolea ukiikwaji wa haki hizo ni katika kipindi
cha miezi sita iliyopita magazeti matano yemefungiwa ambayo ni Mseto, Mwanahalisi, Mawio, Tanzania Daima na Raia Mwema.
Amesema mbali na kufungiwa kwa vyombo hivyo, waandishi mbali
mbali wamepata misukosuko wakati wakiwa kazini. Baadhi yao ni Halfani Lihundi
wa ITV Arusha, ambaye aliwekwa kizuizini na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya
Arumeru, Alexander Mnyeti.
Mwingine ni Augusta Njonji wa Nipashe ambaye hivi
karibuni aliandika habari za Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na
kukamatwa na kuhojiwa na polisi na baadae kuachiwa kwa dhamana.
Pia waandishi wa Mwananchi, Azam TV na Mtanzania huko Geita
nao walipata msukosuko wakati wakiwa kazini kuripoti rabsha za wanafunzi wa Sekondari
ya Geita hivi karibuni.
Matukio mengine amesema ni pamoja na waandishi Joel Maduka wa
Storm FM na Vallence Robert wa Channel Ten kushambuliwa na polisi wakiwa kwenye
msafara wa Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa huko Geita.
Wengine ni wapiga picha wa Kampuni ya The Guardian Ltd,
Selean Mpochi na John Badi, ambao walinyang’anywa kamera zao wakati wakifanya
kazi zao katika mkutano wa Sheikh Ponda katika hotel ya Iris ya jijini Dar es
Salaam hivi karibuni.
Mukajanga amesema ukiukwaji mkubwa wa uhuru wa waandishi
wa habari amekuwa ni kwa serikali kupitia polisi, wakuu wa mikoa na wilaya.
No comments:
Post a Comment