Kishoka 'TRA' akamatwa...soma habari kamili na Matukio360..#share

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) Novemba 03, 2017, ilifanikiwa  kumkamata, Dunia Athumani Tema mkazi wa Buguruni, Dar es Salaam kwa tuhuma za kujifanya Mtumishi wa TRA na kutoa huduma kwa mteja ndani ya  Ofisi ya TRA Kariakoo – Gerezani Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi  wa Mamlaka ya Mapato Tanaznia (TRA), Richard Kayombo.

Mara baada ya kukamatwa mtuhumiwa huyo alifikishwa katika Kituo cha Polisi  kilichopo Msimbazi, Dar es Salaam na kufunguliwa RB ya
MS/RB/9263/17,

KOSA: KUJIFANYA MTUMISHI WA UMMA (TRA).

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inatoa wito kwa wananchi wote kutoa taarifa mara moja katika Vituo vya Polisi vilivyopo karibu, Ofisi za TRA zilizopo karibu au kupiga simu namba 0800780078 au 0800750075 endapo watakuwa na mashaka
na mtu yeyote anaye wahudumia.

Pia Mamlaka inawasisitiza wananchi wasikubali kupewa huduma zozote na mtu wanayemtilia mashaka.

TRA inapenda kuwakumbusha kwamba, watumishi wake wote wanapaswa kuvaa au kuwa na kitambulisho chenye majina na cheo wanapokuwa wanatimiza majukumu yao ya kila siku mahali popote.
‘Pamoja Tunajenga Taifa Letu’
Imetolewa na;

Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
Makao Makuu.

12/11/2017.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search