Trump, Kim Jong-Un watunishiana misuli...soma habari kamili na Matukio360..#share
VITA vya maneno baina ya Rais wa
Marekani Donald Trump na Korea Kaskazini Kim Jong-Un vimerejelea tena kufuatia mpango wa nyuklia wa
Korea Kaskazini.
Rais wa Marekani Donald Trump (Kushoto) na Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong-un (Kulia)
Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ya Korea Kaskazini imemuita rais Donald Trump kuwa "mchochezi
wa vita na mzee" na kusisitiza kuwa haiwezi kamwe kuachana na mipango yake
ya nyuklia.
Rais Trump alijibu kwa kuandika katika mtandao wake wa kijamii
wa Tweeter kuwa, anashangaa ni kwa namna gani Kiongozi wa Korea Kaskazini
anamuita mzee.
Kwa maneno yake, rais Trump amesema kuwa hatamuita Rais Kim
Jong-un, kuwa mtu "mfupi na mnene".
Alisema kuwa atajaribu siku moja kuwa rafiki wa karibu wa rais
huyo wa Korea Kaskazini.
Trump awali alimkejeli kiongozi huyo mkuu wa Korea Kaskazini,
kwa kumuita mwendawazimu na 'mtu wa kuunda zana za roketi'.
No comments:
Post a Comment