Wazazi wanafunzi wajawazito kuswekwa rumande saa 48...Soma habari kamili na Matukio360..3#share
WAKUU wa wilaya na shule mkoani Rukwa
wameagizwa kuwakamata na kuwaweka ndani kwa saa 48 wazazi wa wanafunzi watakaopewa
ujauzito.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa huo
Joachim Wangabo, baada ya kusomewa taarifa ya Shule ya sekondari Kirando, wilayani
Nkasi iliyobainisha wanafunzi saba kupata ujauzito kwa kipindi cha Januari hadi
Oktoba, 2017.
Amesema kumekuwepo na tabia ya kumalizana kienyeji
na matokeo yake watuhumiwa kutofikishwa sehemu husika ili waweze kuwajibishwa.
“Mwalimu mkuu unapogundua mwananfunzi
ana mimba mweke pembeni ita wazazi wake, washirikishe polisi wawachukue wawekwe
ndani kwa muda wa saa 48 hadi hapo watakapomtaja Muhusika wa mimba hiyo,
ukifanya hivyo mara kadhaa mabadiliko yatatokea,” amesisitiza
Aidha amezitaka shule zote atakazo tembelea
katika ziara yake ya kujitambulisha, zihakikishe zinabainisha hatua
zilizochukuliwa dhidi ya watu wanaotuhumiwa kuwajaza wanafunzi ujauzito.
Mkuu huyo wa mkoa alikuwa ametembelea shuleni
hapo kwa ajili ya kukagua ujenzi wa maabara na kuongea na wanafunzi.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Erneo Mgina, amesema kati ya wanafunzi saba
waliopata ujauzito wanafunzi watatu ni wa “A – Level” na wanne ni wa “O –
Level” na kueleza kuwa wengi wao hupata mimba wakati wa likizo na huwabaini
pale tu wanaporudi shule na kuwapima.
No comments:
Post a Comment