Kitilya, wenzake waendelea kusota rumande...soma habari kamili na Matukio360..#share
Na mwandishi wetu
HARRY Msamire Kitilya ambaye ni mwenyekiti wa kampuni
inayoshughulikia uwekezaji wa mitaji na
dhamana (Egma) na waliokuwa maofisa wa benki ya Stanbic, Shose Mori Sinare na
Sioi Graham Solomon wanaendelea kusota rumande kutokana na upelelezi wa kesi inayowakabili
bado haujakamilika.
Harry Kitilya katika akiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
Leo wakili wa
serikali mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,
Godfrey Mwambapa kuwa upelelezi wa kesi
hiyo bado haujakamilika. Pia amedai bado wanasubiri awamu ya pili ya upelelezi kutoka
nchini Uingereza.
Hakimu Mwambapa ameahirisha
kesi hiyo hadi Novemba 10, 2017 kwa
ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la.
Kesi
hiyo inasikilizwa na Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Cyprian Mkeha.
Awamu
ya kwanza ya vielelezo hivyo kutoka
nchini Uingereza vimepokelewa na
vinasubiriwa vya awamu ya pili.
Washtakiwa
hao wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama, kujipatia fedha kwa njia ya
udanganyifu na kutakatisha fedha.
Wanadaiwa
kutenda makosa hayo kati ya Machi 2013 na Septemba 2015 wakati wa mchakato wa
mkopo wa dola za Marekani milioni 550 kwa
serikali ya Tanzania kutoka Benki ya Standard Uingereza.
Wanadaiwa
kuwa Machi 2013 jijini Dar es Salaam
walijipatia Dola za Marekani milioni 6 wakionyesha kuwa fedha hizo zilikuwa ni malipo
ya ada ya uwezeshaji upatikanaji wa mkopo
na zililipwa kupitia Kampuni ya
Egma T Ltd.
Washtakiwa hao wanadaiwa
kutakatisha fedha kwa kuhamisha, kuchukua na kuweka kiasi cha Dola za
Marekani milioni 6 katika akaunti
tofauti tofauti za benki.
Kati
ya Machi 2013 na Septemba 2015,
wanadaiwa kuwa waliweka pesa hizo katika
akaunti mbalimbali zilizomilikiwa na kampuni ya Egma na kwamba walipaswa kufahamu
kuwa pesa hizo ni mazao ya uhalifu wa kughushi.
No comments:
Post a Comment