Okwi awahakikishia Simba ubingwa...Soma habari kamili na Matukio360...#share
NA MWANDISHI WETU
STRAIKA wa Simba, Emanuel Okwi amewaambia mashabiki wa
timu hiyo wasiwe na wasiwasi na ubingwa kwani anamini taji la Ligi Kuu Tanzania
Bara msimu huu litatua Msimbazi.
Emanuel Okwi
Mshambuliaji huyo raia wa Uganda alisema alitoa kauli hiyo mara
baada ya kumalizika kwa mchezo ambao Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi
ya Mbeya City juzi Uwanja wa Sokoine Mbeya.
Ushindi huo uliirejesha Simba katika uongozi wa ligi na
kuishusha Azam iliyoichapa Ruvu Shooting bao 1-0 Jumamosi iliyopita katika
nafasi ya pili kutokana na kigezo cha tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa
licha ya timu hizo kulingana pointi 19.
Akizungumza jijini hapa,Okwi amesema ushindi walioupata
umewazidishia morali ya kuendelea kufanya vizuri ili hatimaye
"Lengo lilikua kupata ushindi ugenini haijalishi
tumechezaje, tumefanikiwa kupata alama tatu ndio muhimu kwetu.
“Kurejea kwetu kileleni kumezidisha kiu yetu ya kuchukua ubingwa
msimu huu,nawaomba mashabiki wa Simba waendelee kutuunga mkono na sisi tunapambana
kwaajili ya kuwapa furaha,”alisema Okwi.
No comments:
Post a Comment