Magufuli, Mseveni waishutumu ICC...Soma habari kamili na Matukio360..#share

RAIS John Magufuli na Rais wa Uganda Yoweri Mseveni wamelaani uamuzi uliotolewa na   Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC), kumuagiza mwendesha mashtaka wa mahakama hiyo kuanzisha uchunguzi dhidi ya mgogoro wa Burundi.
RAIS John Pombe Magufuli akipita kwenye gwaride la Kimya lililoandaliwa kwa heshma na Jeshi la Uganda mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini Uganda na kurejea nchini. 
Akizungumzia uamuzi huo Rais Mseveni ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), amesema ICC imeingilia EAC kabla ya kuwahusisha viongozi wa Jumuiya hiyo, jambo ambalo siyo sahihi na linarudisha nyuma juhudi za kutafuta amani ya Burundi.
Kwa upende wake Rais Magufuli amesema hatua hiyo inarudisha nyuma hatua zilizochukuliwa na EAC ambayo iliunda Kamati ya Usuluhishi ya mgogoro huo inayoongozwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamini Mkapa.
Ameongeza kuwa hali ya Burundi siyo mbaya kama inavyotangazwa kwa kuwa wakimbizi wengi waliokuwa Tanzania wamerejea nchini kwao na wengine wanaendelea kurejea.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipita kwenye gwaride la Kimya lililoandaliwa kwa heshma na Jeshi la Uganda mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini Uganda na kurejea nchini. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mke wake Mama Janeth Magufuli wakifurahia ngoma ya asili iliyokuwa ikipigwa na watoto wa nchini Uganda katika eneo la mpakani la Mutukula kabla ya kurejea nchini. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mpakani mwa Tanzania na Uganda (Mutukula) kuhusu ujenzi wa barabara ya Kutoka Miziro hadi Mutukula bila kupitia wilayani Misenyi. Pembeni yake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akisikiliza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na viongozi wakuu wa Majeshi ya Uganda mara baada ya kumaliza ziara yake nchini Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wananchi wa mpakani  Mutukula upande wa Uganda mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku tau nchini Uganda. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wananchi wa mpakani  Mutukula upande wa Uganda mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku tau nchini Uganda. PICHA NA IKULU.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search