Makonda azidi kupambana na wauza dawa...soma habari kamili na Matukio360..#share

Na mwandishi wetu
MKUU wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataka mabaharia nchini kuisaidia serikali kwa kutoa taarifa  za dawa za kulevya na mali za magendo  zinazopitishwa na kuingia bila kufuata utaratibu hasa  baharini.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda

Ametoa wito huo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua Mafunzo ya Sheria ya Kazi kwa mabaharia ya mwaka 2006 na Marekebisho  yake “Maritime Labor Convention 2006 as amended”  kwa Chama cha Mabaharia Tanzania (TASU).

Katika ukanda wa Kiuchumi wa Bahari, Makonda amewaahidi mabaharia hao wazawa kuwa atahakikisha wanapata upendeleo wa kupata  ajira  katika  Ukanda wa Kiuchumi wa Bahari ili waweze kusaidia kutoa taarifa zinazohusiana na dawa za kulevya ama mali za magendo  zinazopitishwa bila ya kufuata utaratibu .

Pia amewaaeleza wananchi kuwa wana haki ya kudai haki  ya maendeleo ila kwa wale tu wanaolipa kodi na  atakapokutana na rais Magufuli wakati akimpa taarifa za mkoa wa Dar es Salaam atampatia taarifa  hizo na za chama hicho cha TASU.

Makonda amesema  hayo baada ya Baharia, Aloyce Mpazi kusoma risala kwa niaba ya  TASU  ambapo imepongeza kutambuliwa kwa vyeti vya mabaharia wahitimu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI)  na kwamba hiyo inawasaidia  mabaharia kupata fursa ya kutambuliwa, kuajiriwa na kufanya kazi duniani kote.

Pia inasaidia kupanuka kwa wigo wa ajira kwa mabaharia wa kitanzania ndani na nje ya nchi  na kuongezeka na kukua kwa biashara ya bahari (Shipping Business) katika nchi yetu hasa shughuli za bandari na wadau wake.

Mpazi alidai kuwa hayo yanayotokana na serikali ya Tanzania kuhakikisha inaibakisha Tanzanika katika orodha ya shirika la bahari duniani (Internatinal Maritime Organization - IMO) ya nchi zilizokidhi mabadiliko ya matakwa ya sheria ya mafunzo kwa mabaharia, Standard Training and Certification of Watch Keeping (STCW 2010), Manila amendment” maarufu kama “IMO White List”.
Amesema  kuishi kibaharia ni kudumisha miiko na maadili ya kibaharia na kwamba hiyo imechangia kwa njia moja au nyingine kuifanya Tanzania iwemo kwenye “White List” ya IMO.

Kwa takwimu za usafirishaji za dunia zinaonesha kuwa zaidi ya 98% ya shehena kubwa na nzito kutoka sehemu moja kwenda nyingine duniani zinategemea uchukuzi kwa njia ya maji.

Takwimu hizi zinadhihirisha jinsi ambayo fani ya ubaharia ilivyo na fursa pana za ajira kwani uchukuzi huu unafanywa kwa njia ya meli zinazosafiri kuunganisha mabara yote duniani.

 Hii inamaanisha kuwa mabaharia wanahitajika sana si tu hapa nchini lakini zaidi duniani kote, hasa kwenye nchi zenye makampuni makubwa ya meli.

Hivyo chama hicho kina kazi ya kuwakusanya mabaharia Tanzania nzima, kuwahimiza wajiunge katika chama na kuwalea katika misingi na maadili ya kibaharia ili kulinda na kuhifadhi sifa nzuri ambayo ndiyo silaha kubwa ya kuiweka nchi yetu katika rekodi bora ya uchukuzi kwa njia ya maji na hivyo kuzidi kuweka mazingira mazuri kwa mabaharia wetu kupata ajira kwa wingi.


Kwa kuwa nchi ambazo mabaharia wake wanatuhumiwa kwa ukosefu wa maadili, kusababisha au kuhusika katika ajali za majini mara kwa mara na matatizo mengine yanayofanana na hayo, nchi hizo hupata shida sana mabaharia wake kupata ajira katika meli hasa za kimataifa ambazo mishahara yake ni mikubwa.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

1 comment

  1. I mac really excited about Tom Servo and Crow. They are hilarious! Thank you for featuring Hero Lost today. Star Wars will always be a big influence for me. I think Empire Strikes Back was the first movie I ever saw in the theater. Have a great week Alex :) Soma delivery

    ReplyDelete

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search