Waziri mkuu awaonya askari polisi...soma habari kamili na Matukio360..#share
Na mwandishi wetu, Dodoma
SERIKALI imewaonya askari
polisi kuacha vitendo vya kupigia raia kiholela na bila kuzingatia taratibu na
maelekezo halali kutoka vyombo husika.
Waziri mkuu, Kassim Majaliwa akijibu maswali ya hapo kwa hapo
Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni
Dodoma na Waziri mkuu Kassim Majaliwa alipokuwa akijibu maswali ya hapo kwa hapo kutoka kwa wabunge.
Akijibu swali kutoka kwa
mbunge wa Kilwa, Modest Ng’ombare aliyetaka kujua kama serikali ipo tayari
kuwalipa fidia baadhi ya masheikh kutokana na kupigwa na kujeruhiwa wakiwa msikitini na askari polisi mwezi Julai, 2017.
"Mojawapo ya jukumu la
jeshi la polisi ni kulinda raia na mali zao, sasa ikitokea watu wamejeruhiwa au
kupigwa… jambo hilo linategemeana. Kama askari kafanya hivyo binafsi ni kosa na
atachukuliwa hatua za kisheria. Na kama ni maagizo kutoka vyombo sahihi hilo
linautaratibu wake wa jinsi ya kulishughulikia," alijibu waziri mkuu.
Akifafanua zaidi amesema
askari polisi hatakiwa kumpiga raia na zaidi ni kumlinda na kuhakikisha usalama
wake
Kuhusu muda wa kuwapo wafanyakazi
wa kigeni nchini, waziri mkuu amesema sera inaelekeza wawepo kwa miaka miwili
na kutoa utaalam(ujuzi) kwa watanzania.
"Hata hivyo sheria
inaruhusu kumuongezea miaka miwili ikibainika kuwa watanzania bado hawajapata
ipasavyo ujuzi kutoka kwa huyo mfanyakazi wa kigeni. Pia sheria hiyo inaelekeza
mashirika na makampuni ya kigeni kuwa na kitengo maalum cha kutoa utaalam kwa
watanzania." amesema
Kuhusu serikali kutenga
fedha maalumu ya kununua taulo za wanafunzi wa kike, Waziri mkuu Majaliwa
amesema serikali ipo katika mchakato wa kutatua tatizo hilo na kwamba kwa
kuanzia tayari kila shule ina mwalimu wa kike anayehusika moja kwa moja na
masuala ya ndani ya wanafunzi wa kike.
Kuhusu kukabilina na mabadiliko tabia nchi, waziri
mkuu amesema serikali inakabiliana na suala hilo kupitia sheria ya mazingira
inayoelekeza kutoa elimu kwa jamii kuhifadhi mazingira popote walipo.
No comments:
Post a Comment