Wizara ya Maji, Tanesco kuvunjwa...soma habari kamili na Matukio360..#share
Na
mwandishi wetu
RAIS
Dk John Magufuli ameagiza jengo la makao makuu ya shirika la umeme(Tanesco)
na lile la wizara ya maji lililopo Ubungo kuwekewa alama ya X ili kuvunjwa.
Makao Makuu ya Tanesco
Ametoa agizo
hilo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa katika ziara ya kukagua ujenzi wa
daraja la ghorofa tatu makutano ya
barabara eneo la Ubungo
"Ikiwezekana
leo au kesho muweke x katika jengo la Tanesco na lile la wizara ya maji ambapo
ukuta wake upo sehemu ya ndani ya barabara. Sheria ni msumeno hata serikali
ikifanya kosa inasurubiwa na hata raia akijenga kwenye hifadhi ya barabara anasurubiwa," amesema rais na kuongeza
"Sheria
ya hifadhi ya barabara ilianza tangu mwaka 1932 ikafanyiwa mabadiliko mwaka 1959,1963
na 1997 ukubwa wa barabara Morogoro kutoka mjini ni mita 22.5 kwa 22.5."
No comments:
Post a Comment