Mwanasheria ataka wanasiasa 'uchwara' wapuuzwe...soma habari kamili na Matukio360..#share

Na Salha Mohamed

WANANCHI wametakiwa kuwapuuza wanasiasa wanaopinga miradi ya serikali na kwamba wanajali maslahi binafsi na si hamaendeleo ya taifa.

Wakili wa kujitegemea, Leonard Manyama  akizungumza  na waandishi wa habari(hawapo pichani) kutoa tamko la kuunga mkono uongozi wa rais John Magufuli katika kipindi cha miaka miwili 

Wito huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na wakili wa kujitegemea, Leonard Manyama wakati akitoa tamko la kuunga mkono uongozi wa miaka miwili wa rais John Magufuli

"Tuwapuuze wanasiasa wanaopinga miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa na serikali kama ujenzi wa treni ya kisasa, mradi wa umeme wa Stiglas na ununuzi wa ndege, "amesema.

Amesema miradi hiyo ina manufaa  kwa taifa na kuiunga mkono serikali hata kama inakopa fedha za miradi hiyo.

" Tuwapuuze wanasiasa wanaotuaminisha kuwa serikali hii ni mbovu eti hakuna fedha mifukoni, fedha zitapatikana kwa kufanya kazi kwa bidii na si kwa madili haramu, "amesema.

Manyama amesema wapo  baadhi ya wanasiasa wanaokwepa kulipa kodi huku wengine walikuwa serikalini na kutumia nafasi zao kujilimbikizia mali, mashamba na kujibinafsisha au kuuza Viwanda.

" Hawa ni watu hatari sana si wa kuwaunga mkono hata kidogo wanapaswa kuolewa a kupuuzwa.. .. Hadi 2020 tutawajua wanasiasa wazalendo na wanasiasa matapeli na wenye nia binafsi, "amesema.

Amesema rais Magufuli amekuwa akipambana na rushwa, ufisadi, kudhibiti ukwepaji wa kulipa kodi, kuimarisha kwa vita dhidi ya biashara haramu ya dawa za kulevya, ujangili na mapambano dhidi ya rasilimali kama madini.

Amesema hatua hiyo ndiyo imesababisha kupotea kwa fedha zilizokuwa zikipatikana kwa njia ya haramu huku wanasiasa wakidai kupotea kwa fedha ni kutokana na uongozi mbovu wa Rais Magufuli na serikali yake.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search