NEC kutangaza uchaguzi majimbo mawili, kata tano zilizo wazi...soma habari kamili na Matukio360..#share








Na mwandishi wetu
TUME ya taifa ya uchaguzi(Nec) imepokea taarifa rasmi ya kuwapo kwa majimbo mawili na kata tano zilizowazi kufuatia wabunge na madiwani kujiuzulu na wengine uteuzi wao kutenguliwa na mahakama.
Watendaji wa kuu wa NEC wakipitia baadhi ya nyaraka kuhusu uchaguzi

Kufuatia hali hiyo NEC inatarajia kutangaza marudio ya uchaguzi mdogo katika majimbo  na kata hizo
Soma taarifa kamili 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imepokea taarifa kutoka kwa Mhe. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiitaarifu kuwepo kwa nafasi wazi ya Ubunge katika Jimbo la Singida Kaskazini kufuatia Ndugu Lazaro Samwel Nyalandu kuvuliwa Uanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na hivyo kupoteza sifa ya kuwa Mbunge. 
Aidha, kwa mujibu kifungu cha 113(1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, Tume imepokea Hati ya Mahakama Kuu ya Tanzania ikithibitisha uamuzi wa Mahakama hiyo juu ya kutengua matokeo ya Uchaguzi wa Mbunge wa Jimbo la Longido ambalo Ndugu Onesmo Ole Nangole alikuwa ni Mbunge.
Wakati huo huo Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa kwa kutumia mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, ameitaarifu Tume uwepo wa nafasi wazi za Madiwani katika Kata tano zilizopo katika Halmashauri mbalimbali.
Kwa kuzingatia masharti ya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi itatoa ratiba ya Uchaguzi Mdogo wa kujaza nafasi wazi za Majimbo na Kata hizo hapo baadae.
Majimbo na Kata zilizo wazi ni kama ifuatavyo:-
Jedwali Na. 1: Majimbo yaliyowazi
NA.
MKOA
HALMASHAURI
JIMBO
1.
Singida
Halmashauri ya Wilaya ya Singida
Singida Kaskazini
2.
Arusha
Halmashauri ya Wilaya ya Longido
Longido

Jedwali Na. 2: Kata zilizowazi
NA.
MKOA
NA.
HALMASHAURI
NA.
KATA
1.
Kagera
1.
Halmashauri ya Wilaya ya Ngara.
1
Keza
2.
Arusha
2
Halmashauri ya Jiji la Arusha
2
Kimandolu
3.
Pwani
3.

Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe.
3
Kurui
4.
Tabora
4.
Halmashauri ya Wilaya ya Tabora
4
Bukumbi
5.
Tanga
5.
Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe.
5
Kwagunda



Jaji (R) Semistocles S. Kaijage
MWENYEKITI
 TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

16 NOVEMBA, 2017

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search