TFF kufungua mashtaka dhidi ya mitandao ya kijamii...soma habari kamili na Matukio360..#share
Na Mwandishi Wetu
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limemwagiza mwanasheria wake
kufungua mashtaka kwa wale waliosambaza taarifa kwenye mitandao ya kijamii
kuichafua taasisi hiyo. Matukio360 haimo katika sakata hilo.
Katikati ni Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Hatua hiyo inakuja baada ya jana kusambaa taarifa za kuwatuhumu viongozi wa TFF kuongeza
posho kwa wajumbe wa kamati ya utendaji pamoja na kuanzisha malipo ya mishahara
kwa rais na makamu wake.
Agizo hilo limetolewa leo jijini Dar es Salaam na Kaimu Katibu Mkuu wa
TFF Wilfred Kidao alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
“Ninamwagiza mwanasheria wetu kufungua mashtaka kwa wale waliosambaza
ujumbe kwenye mitandao ya kijamii wenye lengo la kuichafua taasisi,” amesema
Kidao.
Aidha amekanusha taaarifa hizo kwa kusema kuwa viwango vya posho za
vikao vya Kamati ya Utendaji havijawahi kujadiliwa wala kubadilishwa.
Ameongeza kwamba wajumbe wa kamati ya utendaji wanawezeshwa sh.milioni
1.5 kwa miezi mitatu ili kuwasaidia katika kutgrkrleza majukumu yao.
Akitolea ufafanuzi kuhusu malipo ya Rais na Makamu wake, amesema suala
hilo halikufikiwa mwafaka na kamati ya utendaji hivyo walishauri rais ahudumiwe
na TFF kama ilivyo kwa marais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika
(CUF).
Pia Kidao amebainisha kuwa Rais wa TFF Wallace Karia alikataa kwa
kusema, anaamini sio wakati mwafaka wa yeye kuchukua posho hadi taasisi
itakapokaa vizuri na taratibu zote kufuatwa
.
No comments:
Post a Comment