Nusu wanafunzi elimu ya juu wakosa mikopo…Soma habari kamili na Matukio360...#share
Na Salha Mohamed
MTANDAO wa Wanafunzi Tanzania(TSNP) umesema nusu ya wanafunzi wenye sifa na waliodahiliwa na vyuo vya elimu ya juu nchini wamekosa mikopo na kurudi nyumbani.
Mkurugenzi wa Idara ya haki mtandao wa wanafunzi Abdul Nondo(katikati)
akitoa msimamo wa taasisi hiyo katika suala la utoaji wa mikopo kwa wanafunzi
wa elimu ya juu leo jijini Dar es Salaam.
Pia umetoa siku tano kwa Serikali kuhakikisha wanatoa tamko na
azimio walioamua juu ya wanafunzi wenye sifa, waliokosa mikopo ili
waweze kudahiliwa na kuanza masomo.
Hayo yamebainishwa Dar es Salaam leo na Mkurugenzi wa Idara ya
Haki TSNP, Abdul Nondo wakati akizungumza na waandishi wa habari na kutoa
msimamo wa mtandao huo katika suala la utoaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya
juu.
Amesema serikali ilipanga kutoa sh bilioni 427 kwa mwaka wa
masomo 2017/2018 kwa wanafunzi wote nchini ambapo kwa mwaka wa kwanza ilipanga
kutoa sh bilioni 108.8 kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza sawa na wanafunzi
30,000.
“Wanafunzi waliodahiliwa mwaka huu ni elfu 61, hii inamaanaisha
kwa vyovyte vile wanafunzi elfu 31 kati ya elf 61 walioomba mkoo walipaswa
kukosa mkpo, tunashangazwa na Bodi ya mikopo kupitia mkurugenzi wake kuwa
walichambua wasiokuwa na sifa lakini wanafunzi hao hawakukosa mkopo kutokana na
vigezo bali ni idadi iliyowekwa,”amesema.
Amefafanua kuwa serikali inapaswa kufanya kama ilivyofanya
sekondari kwa kulipa ada ya kila mwanafunzi huku mzazi akigharamia
chakula na malazi.
“Hadi jana tumepata taarifa kuna baadhi ya vyuo wanafunzi
wanarudi nyumbani kutokana na kukosa ada na hawaruhusiwi kuingia darasani kwani
hawajasajiliwa na chuo,”amesema.
Kwa
upande wake mmoja wa wanafunzi wa mwaka wa kwanza mkazi wa mkoani Kilimanjaro,
Denis Shirima amesema si kwamba bodi ya mikopo imewanyima mkopo kutokana na
kukosa vigezo.
Amesema ameambatanisha nyaraka zote zinazomthibitishia kuwa yeye
ni Yatima na anapaswa kupata mkopo lakini amekosa.
"Najua wapo wengi kama mimi wamekosea mkopo mkono na hawana
ndugu hapa jijini, wengine wmejishikiza tu kwa marafiki zao akitegemea mkopo lakini
amefika amekuta hajapata, "amesema.
Amesema wapo wanafunzi wanaorudi majumbani mwao kutokana a
kushindwa kulipa ada jambo linalosababisha kukosa kudahiliwa chuoni n kukosa
masomo.
" Mwanzo tulipofika chuo tulikuwa tunaibia ibia tu kuingia
darasani ili tupate mwanga wa kile tulichoomba kusoma lakini sasa hivi
haruhusiwi kuingia hadi uwe na kitambulisho na hadi kupewa lazima uwe umelipa
ada, "amesema.
Amesema anatarajia kupata kauli kutoka kwa waziri wa elimu,
Profesa Joyce Ndalichako kwani hadi sasa hawana mwelekeo huku masomo yameanza
vyuoni.,"amesema.
Naye mwanafunzi wa Maka wa pili katika chuo cha Elimu ya
Biashara (CBE) Aziza Rashidi amesema mwaka wa kwanza aliomba mkopo lakini
alikosa ambapo alifika bodi ya mikopo ambapo maofisa wa bodi hiyo walishangaa
kukosa mkopo kwani alikuwa anavigezo vya kupata.
"Mwaka wa kwanza nimesoma kwa kuomba na kukupa kwa ndugu
ndugu na jana jana na sasa hivi na dawa nikaomba tena mwaka huu sijapata sina
wazazi nimeweka dhamana vyeti vyangu ili nipate hela niseme na sijapata mkopo,
"amesema.
TUNATOA MIKOPO YA HARAKA YA € 15000 Hadi $ 72000 KIASI CHOCHOTE CHA UCHAGUZI WAKO NA 2-4
ReplyDeleteSAA YA HUDUMA YA MAFANIKIO YA KUFANIKIWA NA 2% VIWANGO VYA RIBA KWA BIASHARA
NA BINAFSI
MADHUMUNI SASA TUMIA NA UJUMBE WA BARUA KWA:
philipmorganloanservice00@gmail.com
JAZA NA URUDI
Jina:
Kiasi cha Mkopo:
Muda:
Jinsia:
Nchi:
Lengo:
Namba ya simu ya mkononi:
JIBU LAKO NI LAZIMA MARA MOJA